Kaimu Mkurugenzi wa MNH Profesa Lawrence Museru (kushoto) akimueleza jambo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mara baada ya kutembelea jengo hilo
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja nje ya jengo la Maternity Block Two na baadhi ya Wakurugenzi wa idara wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, aliyesimama katikati kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa MNH Profesa Lawrence Museru.
Waziri Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Profesa Lawrence Museru wakitoka ndani ya jengo hilo la wazazi “ Maternity Block Two” leo Apriil 18, 2016.
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa lengo la kukagua ukarabati wa jengo la wazazi- Maternity Block Two - ambao bado unaendelea.
Akizungumza mara baada ya kutembelea jengo hilo Waziri Ummy amesema anaridhishwa na zoezi hilo la ukarabati ambapo amesisitiza kuwa ni faraja sasa kuona hakuna mama mjamzito anayelala chini.
“ Kuwepo kwa jengo hili ni faraja kwa kina mama nafurahi kuona ukarabati unaendelea vizuri na upo katika hatua nzuri kwakweli mnastahili pongezi kwani mnafanya kazi nzuri” amesema Waziri Ummy.
Maternity Block Two mpaka sasa kuna jumla ya vitanda 63 ambavyo vinatumika na wakina mama wanaendelea kupatiwa huduma.

No comments:
Post a Comment