ANATOLIA KOKUSHUBILA BARONGO
1944 - 2015
Mwaka mmoja umepita tangu mama yetu mpendwa ulipoitwa na Mwenyezi Mungu tarehe 15 Aprili, 2015 na kupumzishwa Kanyigo, Misenyi-Kagera tarehe 20 Aprili, 2015.
Umetuacha katika majonzi makubwa lakini tukiwa na matumaini ya kuonana tena tukimtukuza Mungu pamoja na Malaika na Watakatifu wote Mbinguni.
Hatutasahau upendo, ucheshi, upole, hekima, bidii yako, moyo wa kujitoa kuwahudumia wengine na kutokupenda makuu.
Unakumbukwa na Mume wako mpendwa Lambert, watoto wako Edmund, Vivien, Osbert, Comfort, Andrew na Atuganyila, wakwe zako Menrad, Justa na Mercy wajukuu zako Rehema, Mwesiga na Oleen, ndugu, marafiki na majirani.
Familia itatoa Sadaka ya shukrani katika Ibada itakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 17 Aprili, 2016 Saa Moja asubuhi katika Kanisa la KKKT-Tangi Bovu-Mbezi Beach.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele umwangazie, Apumzike kwa Amani,Amina.
No comments:
Post a Comment