Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SERIKALI imesema kuanzisha kambi za kufanya oparesheni kwa watoto wenye migongo wazi na vichwa vikubwa itasaidia kuokoa maisha ya watoto hao kutokana na wazazi wao kushindwa kumudu gharama za oparesheni hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati makababidhiano ya magari kwa ajili ya kambi hizo, Mwakilishi wa Waziri wa Afya na Maendeleo jamii jinsia, Watoto , Mkuu wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa Mfuko wa GSM wametambua matatizo ya watoto hao na kuamua kutoa sehemu yao katika kuhakikisha watoto hao wanafanyiwa oparesheni.
Makonda amesema kambi hizo wazazi watapeleka watoto tu ambayo ndio gharama yab kufanya watoto wao wafanyiwe oparesheni ya matatizo yao.
Amesema kuwa watu walikuwa wanafikiria ndani ya bajeti tu bila kuangalia wadau wana uwezo gani na kusababisha mambo kurudi nyuma kwa GMS wameonyesha njia katika kufanya ufadhili wa oparesheni hiyo.
‘’Naamini watoto hao watakuwa kuwa watumishi wenye maadili kutokana na matatizo waliopata na watu wengine wakahangaikia hivyo hawawezi kuwa mafisadi kwa kujua atachochukua kuna watu wanahitaji’’amesema Makonda.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk.Othman Kiloloma amesema kuwa daktari wenye utaalamu huo ni daktari tisa tu kati ya hao nane ni Hospitali ya Taifa Muhimbili na mmoja Hospitali ya Bungando.
Dk.Kiloloma amesema kufanya operesheni ya mtoto mmoja ni sh. Laki saba hadi milioni moja ambapo baadhi wanashindwa kumudu hivyo ufadhili wa GSM utafanya kuweka kambi na kutoa huduma hiyo bure kwa watoto pamoja na kutoa elimu kwa baadhi ya daktari juu ya oparesheni ya watoto wenye migongo wazi na vichwa vikubwa.
Afisa Mawasiliano wa GSM , AKhalfan Kiwamba amesema kuwa wanatambua matatizo ya watoto hao na kuamua kufanya ufadhili ili waweze kufanyiwa oparesheni hiyo.
Amesema kambi hizo awamu ya kwanza itakuwa Mkoa wa Mwanza Aprili 27 hadi 30, Shinyanga Mei 2 hadi 4, Singida Mei 6 hadi 8, Dodoma 10 hadi 13, Morogoro Mei 15 hadi 17 .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikata na utepe kuzindua magari ambayo yametolewa na Mfuko wa GSM kwaajili ya kusidia kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa pamoja na watoto wenye migongo wazi katika kambi itakayofanyika katika mikoa ya Mwanza Aprili 27 mpaka Aprili 30, Shinyanga Mei 2 mpaka 4, Singida Mei 6 mpaka Mei 8, Dodoma Mei 10 mpaka 13 na Morogoro 15 mpaka 17.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika uzinduzi wa kambi ya upasuaji ya watoto wa wenye vichwa vikubwa na watoto wenye matatizo ya mgongo wazi ambapo Mfuko wa GMS kushirikiana na Taasisi ya Mifupa (MOI) katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili wataanza kambi hiyo katika mikoa ya Mwanza Aprili 27 mpaka Aprili 30, Shinyanga Mei 2 mpaka 4, Singida Mei 6 mpaka Mei 8, Dodoma Mei 10 mpaka 13 na Morogoro 15 mpaka 17. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma na Mkurugenzi wa tiba MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Samwel Swai.
Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kambi ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na watoto wenye Migongo wazi. Kulia ni kuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa GSM, Shannon Kiwamba.
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa GSM, Khalfan Kiwamba akizumgumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na GSM kutoa mchango wake kwa kusaidia watoto wenye matatizo ya Mgongo wazi na watoto wenye vichwa vikubwa. Kusoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa GSM, Shannon Kiwamba.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimpa ufunguo za magari,Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mfuko wa GSM leo katika hospitali ya Muhimbili kwenye kitengo cha MOI jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment