Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amewateua wajumbe wanne wa kamati ya maudhui watakaotumikia kipindi cha miaka mitatu.
Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Idara ya Habari Maelezo ilieleza kuwa uteuzi huo hufanyika kila baada ya miaka mitatu.
Wajumbe wa Kamati hiyo ni Joseph Mapunda ambaye ni mhariri Mtendaji Mstaafu wa Magazeti ya Serikali(TSN) na Mkurugenzi Mstaafu wa Redio Tanzania Dar es Salaam(RTD) Abdul Ngalawa.
Wengine ni Mwandishi wa habari ,Mhadhiri Derek Murusuri pamoja na Mwandishi wa habari ,Mwanasheria , Zainabu Mwatawala.
No comments:
Post a Comment