TWAWEZA, IBM NA BITES & BYTES WAANDAA MKUTANO WA KITEKNOLOJIA MACHI 29 NA 30 MWAKA HUU.
Mkuu wa Utafiti Twaweza, Elivis Mushi.
ASASI isiyo ya kiraia ya Twaweza na Kampuni ya IBM ikishirikiana na Bites &Bytes imeandaa mkutano mkubwa wa Kiteknolojia na uvumbuzi unaoitwa Bites &Bytes ambao utafanyika Machi 29 na 30 mwaka huu katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na mwanzilishi wa
Bites &Bytes, Lilian Madeje wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Liliani
amesema kuwa lengo mkutano huo ni kuhamasisha uendelezaji wa mawazo
mpya pamoja na uvumbuzi wa mawazo mapya ya kibiashara ili aanzishaji
wapya wa mawazo waweze kuwapa mwanya wa kubadilishana mawazo na wadau
wengine ili waweze kushirikiana kwa pamoja.
Pia
Liliani amesema kuwa washiriki 16 wa mechanguliwa kushiriki katika
shindano hilo la ubunifu wa biashara ambapo washiriki hao watashindania
kuwania kitika cha shilingi milioni tano(5,000,000).
Nae
NBV wa benki ya CBA Group, Eric Luyangi amesema kuwa katika shindano
hilo la Software Developers wanalenga kuleta suluhisho la kuwezesha
kufikisha takwimu na tafiti mbalimbali za Twaweza kwa kutumia mitandao
tofauti tofauti.


No comments:
Post a Comment