Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfray Simbeye akizungumza katika mkutano wa Wafanyabiashara wa India juu ya uwekezaji nchini iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe (Kulia) akizungumza katika Mkutano wa Wafanyabiashara wa India juu ya uwekezaji nchini iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyabiashara wa India wakiwa katika meza wakati wa mkutano wafanyabiasha wa nchi hiyo juu ya kushiriki uwekezaji nchini iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SERIKALI imesema itaendeleza mapambano dhidi ya rushwa, ubadhilifu wa fedha za umma, urasimu, uzembe katika ofisi zote za serikali kwa lengo la kukuza na kuimarisha mazingira mazuri na rafiki kwa wafanyabiashara na wawekezaji ili kukuza uchumi na maendeleo ya nchi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana na Jumuiya ya wafanyabiashara wa India (IBF), Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Harrison Mwakyembe alisema kwamba serikali ya awamu ya tano inafanya marekebisho makubwa ya muundo wake na utendaji kazi ili kukabiliana na changamoto za muda mrefu katika Nyanja ya biashara na wawekezaji.
Alisema kuwa India ni mwekezaji mkubwa wa pili nchini Tanzania hivyo ni jukumu la serikali kuhakikisha kwamba mazingira mazuri na rafiki ya biashara kwa wafanyabiashara wote kutoka Asia bila kuingiliwa ovyo na watendaji wa serikali.
“Kweli tumesikia malalamiko ya wafanyabiashara na usumbufu wa maafisa wa serikali hasa askari wa usalama barabarani kudai mpaka kadi za manjano na nimewaahidi serikali ya awamu ya tano itawashughulikia bila kuwaonea aya,” alisema Dk Mwakyembe.
"Naweza kuwahakikishia Rais wa tano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli yeye ni anatembea kwenye maneno yake dhidi ya mapambano ya rushwa nchini ambacho ni kikwazo kwa wawekezaji," alisema.
Alifafanua kwamba mamlaka za ukaguzi kuwa nyingi nchini ni swala ambalo serikali inalitizama kwa jicho makini ili kuleta marekebisho ya kisheria kupunguza usumbufu na kukatisha tamaa wawekezaji na wafannyabiashara nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo wa Wafanyabiashara India, Bw, Gagan Gupta alisema kuwa Tanzania na India kiwango cha biashara kimefikia dola za kimarekani milioni 400 na nchi hizo mbili zimeahidi kuendelea kushirikiana katika mambo ya kiuchumi na kupunguza vikwazo vya kibiashara.
"Jukwaa hadi sasa linakaribu wanachama 108 waliosajiliwa na bado wanaendelea kujisajili na sisi jukumu letu ni kuwaunganisha na mamlaka za serikali zote mbili India na Tanzania,” aliongeza.
Hivi karibuni, Ubalozi wa India hapa nchini ulianzisha visa kwa njia ya kieletroniki na kufuta ada kwa wafanyabiashara wa kitanzania na watanzania wanaotafuta kazi nchini India katika muendelezo wa kukuza mahusiano wa nchini hizo mbili.
No comments:
Post a Comment