KATIBU Mkuu Kiongozi, Mhadisi Balozi John Kijazi(Pichani) amesema makatibu wakuu na manaibu wafanye kazi kwa mujibu sheria na waishi kama viongozi wa umma katika maisha.
Katibu Mkuu Kijazi ameyasema hayo leo wakati wa mafunzo maadili ya viongozi wa Umma kwa Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam,amesema kuwa kama sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma ina matatizo ya utekelezaji wa kisheria kwa viongozi wa umma serikali iko tayari kuyarekebisha.
Amesema mafunzo kwa viongozi wa umma ni muhimu katika kupunguza masuala ya rushwa pamoja na ubadhirifu wa mali za umma.
Aidha amesema kuwa makatibu wakuu na manaibu wafanye kazi kwa kutenda haki kwa waliochini yao kutokana na maadili ya utumishi wa umma.
Nae Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angellah Kairuki amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada zinazofanyika hivi sasa za kukuza na kuinua kiwango cha uwajibikaji na maadili katika utumishi wa Umma kutokana na maadili ya taifa ni moja ya tunu taifa muhimu inayotambulisha Taifa.
Angellah amesema mafunzo waliopata yawe ni chachu ya kasi ya kujenga na kukuza maadili katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Amesema watendaji wakuu wanatakiwa kuwa mfano bora na wa kuigwa kwani serikali imechukua hatua mbalimbali ili kuongeza mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa na ukosefu wa maadili hususani miongoni mwa viongozi wa umma.
No comments:
Post a Comment