Balozi Mdogo wa Uingereza, Matt Sutherland akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na Uingereza na Tanzania kufanya kazi kwa pamoja katika mafunzo haya. Historia yenye kufanana katika sheria na taasisi zetu za kisheria inatoa fursa pana kwa nchi hizi kuweza kufanya kazi na kujifunza baina ya kila mmoja. Mafunzo haya yatawezesha kutoa ujuzi wenye thamani kwa wale watendaji wa mstari wa mbele katika kupambana na makosa makubwa nchini Tanzania.leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Shaban Lila.
Jaji Kiongozi kutoka mahakama kuu ya Tanzania Shaban Lila akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mahakimu watatumia ujuzi na elimu walioipata katika kutatua changamoto ya ucheleweshwaji wa kesi na mashauri mbalimbali, leo jijini Dar es Salaam.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Shaban Lila akimpa cheti chamafunzo ya namna ya kushughulikia makosa makubwa Joachim Tiganga katika hoteli ya White Sands, Mbezi Beach, Dar es Salaam.
Balozi Mdogo wa Uingereza, Matt Sutherland na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Shaban Lila wakiwakatika picha ya pamoja na Mahakimu wafawidhi 14 toka mahakama mbalimbali Tanzania ikiwemo; Kisutu, Kigoma, Arusha, Moshi, Mwanza, Sumbawanga, Temeke, Dodoma, Kinondoni na Mbeya wamehudhuria mafunzo hayo.leo jiji Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)
Na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)
MAHAKIMU nchini wametakiwa kuhakikisha wanatumia vyema mafunzo wanayoyapata katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufasaha hasa katika kuamua kesi kubwa kama za ugaidi, madawa ya kulevya ,ufisadi na utakatishaji wa fedha haramu ili kuiendeleza nchi.
Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Jaji Kiongozi Mahakama kuu ya Tanzania, Shaban Lila wakati akifunga mafunzo maalumu kwa ajili ya kuongeza ujuzi wa kijaji wa kuhukumu makosa makubwa ya kialifu.
Mafunzo yalioandaliwa na serikali ya uingereza kwa kushirikiana na mahakama kuu ya uingereza ambapo amesema mafunzo hayo yatakuwa na msaada zaidi endapo wahusika ambao ni mahakimu watatumia ujuzi na elimu walioipata katika kutatua changamoto ya ucheleweshwaji wa kesi na mashauri mbalimbali.
Mafunzo haya ni ya pili kutolewa kwa Mahakama ikiwa ni kufatiwa kwa mafunzo yaliyokwisha kutolewa mnamo Novemba, 2015 kwa Majaji wa Mahakama Kuu.
Ukanda wa Bahari ya India unakabiliwa na ongezeko kubwa la wasafirishaji wa madawa ya kulevya ambao husafirisha viwango vikubwa vya madawa haramu ya kulevya kuyaleta Afrika Mashariki toka nchi za Afghanistan na Pakistani.
Tangu mwaka 2012 Majeshi ya Kimataisha ya Wanamaji katika ukanda huu yamemudu kudhibiti zaidi ya vyombo vya baharini 44 na kukamata zaidi ya tani 8 za madawa aina ya heroini na tani 30 za madawa aina ya “hashish”.
Ushirikiano katika kazi baina ya Uingereza na Tanzania umefanikisha kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa wasafirishaji wakubwa wa kimataifa wa madawa ya kulevya kote Tanzania na Uingereza Matt Sutherland alieleza na kufafanua kwanini Uingereza inafadhili kazi hizi Tanzania na Uingereza ina mtizamo unaoshabihiana katika kukabiliana na makosa makubwa.
Tunaona kuongezeka kwa wahalifu wa kimataifa wakitumia mitandao ya kimataifa kusafirisha madawa ya kulevya, mazao haramu ya wanyamapori au kuficha wahalifu. Ni kwa kufanya kazi kwa ushirikiano tu ndipo kunaweza tukahakikisha wahalifu hawana mahala pakujificha.
No comments:
Post a Comment