JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YACHANGANUA FEDHA ZILIZOKUSANYWA SERIKALINI.

Share This
Wizara ya Fedha na Mipango leo wamechanganua mapato ya fedha zilizokusanywa serikalini kwa mwezi Desemba hadi Feruari Mwaka huu.

Deni la Taifa zimelipwa kiasi cha  sh.Bilion 81.13
Mikopo ya Elimu ya Juu sh. Bilion 13.683
Mamlaka ya Elimu (TEA) sh. Bilion 2.078
Mamlaka ya Maji vijijini sh.Bilion 7.115
Mradi wa barabara sh. Bilion 58.186 hizi zimegawanywa kwenye makundi mawili ambayo ni Wazara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano sh. bilion 40.73 na Tamisemi bilion 17.456.

Wizara ya Nishati na Madini kwenye upande wa Usambazaji wa Umeme Vijijini (REA) Sh. bilion 20.199 na Mfuko wa Mamlaka ya Reli sh. bilion 2.03.

Na upande wa mfuko wa Jimbo na Halmashauri sh. Bilion 4.503. Fedha za Miradi ya Maendeleo  sh. bilion 166.192.

Kwa upande wa Afya ni  kwenye chuo cha Afya  cha Mloganzila Sh. Bilion 18.



 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servaciaus Likwelile akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na ufafanuzi wa mapato ya serikali na matumizi ya serikali kwanzia mwezi wa Desemba mpaka februali na mgawanyo wa Fedha hizo.
Kaimu kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alfayo Kidata akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kuwashukuru wa Tanzania wanao toa taarifa mbalimbali ambazo zinakosesha mapato ya Serikali, pia amewasihi wananchi wanapo nunua kitu chochote dukani kuomba Stakabadhi(Lisiti) kila wanapo nunua bidhaa.
Pia amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)imekusanya fedha hizo kwa mwenzi Desemba mpaka Februari ambazo zimewekewa matumizi mbalimbali.
Katika kutekeleza ahadi ya Rais Dkt. Magufuli ya Elimu Bure.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Tarishi Kibenga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kuwaomba wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu na waalimu kusoma kwa bidii ili watoe elimu iliyo bora kwa wanafunzi wanao wanaowafundisha. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kuwashuku wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa kukusanya Pesa ambazo zilikuwa zinaliwa na wachache kama kwenye wizara yake pesa zilizotengwa kwaajili kumalizia jengo la  chuo cha Msongazila kumaliziwa kwa haraka ili wanafunzi wa Idara ya Afya kusoma katika hali nzuri.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad