JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WANAUME KUFURAHIA MAFANIKIO YA WANAWAKE.

Share This
Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Agnes Mgongo  akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam leo.

Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
 WANAUME wameshauriwa kushiriki na kufurahia mafanikio ya wanawake kwa kuwa na usawa wa kijinsia na kusaidia kufanikisha malengo na ndoto za wanawake wanaowazunguka katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Agnes Mgongo wakati akizungumza na wandishi wetu jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa wanaume wana nafasi kubwa ya kumsaidia mwanamke kujikwamua katika nyanja za kiuchumi, kiafya hata kijamii kwani ndiye baba, kaka, au kiongozi wa familia.

Agnes amesema Kuwa kutambua umuhimu wa mwanaume katika suala hili, Trumark katika kuadhimisha siku ya wanawake dunianin wameandaa tamasha la Pamoja Tunafanikisha ambalo litahusisha wanaume ili nao waelewe kuwa wana umuhimu mkubwa katika maisha ya mama, dada, Binti na wake zao.

Tamasha la Pamoja Tunafanikisha litafanyika Machi 5, mwaka huu katika Ukumbi wa King Solomoni, eneo la Namanga jijini Dar es salaam ambapo wanaume na wanawake wataungana kusherekea mafanikio ya wanawake na  kutambua changamoto nyingi zinazomkabili mwanamke,  katika kuadhimisha siku hiyo  kutakuwa na  wadau mbalimbali  kutoka nyanja tofauti ili kujadiliana namna ya kuzikabili changamoto hizo  na kuzifanya  kuwa fursa na pia kuwapongeza wanawake ambao wameonyesha njia kwa kujikwamua kiuchumi, jamii na kiafya.

Kampuni ya Trumark imekua ikiadhimisha siku ya wanawake Kwa takribani miaka mitano sasa na tumekuwa na mafanikio makubwa kwani washiriki wengi wamekuwa na mrejesho chanya, nakuongeza mtandao katika shuguli zao mbalimbali.

Agnes amesema maadhimisho yataambatana na burudani kutoka kwa wasanii wa bendi ya mapacha watatu pamoja na chakula cha usiku katika kusheherekea mafanikio ya wanawake,pia anawakaribisha  wanawake pamoja na wanaume kujitokeza kwa wingi ili maadhimisho hayo yalete mafanikio zaidi  katika siku hii muhimu kwa jamii yetu. 
Kwa mawasiliano
Daria Erasto
Afisa Uhusiano
Trumark
+255 716 676665/ 754 095017

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad