JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WAKUFUNZI WATATU WA ELIMU YA WATU WAZIMA WA MIKOA KUVULIWA MADARAKA.

Share This
Kamishina wa Elimu,Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balamsesa akizungumza na waandishi habari (Hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fedelis Mafumiko akizungumza na waandishi habari (Hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Kamishina wa Elimu,Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balamsesa.

Baadhi ya Waandishi habari wakimsikiliza Kamishina wa Elimu,Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balamsesa (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam 

(Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya Jamii).


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii. 
KAMISHINA wa Elimu, Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balamsesa amemuagiza Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fedelis Mafumiko kuwavua madaraka Wakufunzi Wakazi Watatu (3), wa Elimu ya Watu Wazima kutokana na kukiuka utaratibu wa kuchagua wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza kuwaingiza katika Mfumo wa Elimu ya Watu Wazima. 



Profesa Eustella ameyasema hayo leo wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , amesema kuwa wakufunzi hao wamedanganya kutokana na kuingiza huo utaratibu wa kuwapata wanafunzi wa elimu ya watu wazima. 

Amesema kuwa wakufunzi hao wamekuwa wakishirikiana na Halmashauri baada ya kuchagua wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wamefanya vizuri wao kuchukua wanafunzi waliofeli na kuwapeleka katika shule za serikali wakadai kuwa wanafunzi wamechaguliwa katika chaguo la pili. 

Amesema wazazi wamekuwa wanachanganywa na mkanganyiko huo baada ya kuchaguliwa wanafunzi hao wakifika shule wanadaiwa ada wakati serikali imesema bure. 

Wakufunzi waliopata na kadhia hiyo ni Wotugu Mganda (Dar es Salaam), Senorina Kateule (Dodoma),Steward Ndandu Geita na (Mwanza). 

Profesa Eustella amesema kuwa wakufunzi hao wamekuwa wakidandia matokeo ya kidato cha kwanza kwa kufanya upotoshaji kwa wazazi wakati wanafunzi wanaosoma katika elimu ya watu wazima ni hiari kutokana sera ya elimu. 

Wanafunzi ambao wamechaguliwa kwa mwaka huu wamekuwa wakidai ada ya sh. 80,000 hadi 250,000 na ndipo malalamiko yakaanza kwa wazazi baada ya kudaiwa ada hiyo. 

Profesa Eustella, amesema kuwa mmoja wanafunzi katika Mkoa wa Dar es Salaam aliambiwa amefaulu katika chaguo la pili katika shule ya sekondari ya Oasterbay na baada ya kufika wanafunzi wanakuta mambo tofauti kwa kudaiwa ada na kuambiwa awasiliane na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima. 

Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fedelis Mafumiko amesema kuwa watu hao wakivuliwa madaraka wanakuwa walimu wa kawaida wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na kukaimisha nafasi zao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad