JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


CHAWATA KIMEIOMBA SERIKALI KUBORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA MHIMU KWA WATU WENYE ULEMAVU.

Share This
Mwenyekiti wa chama cha walemavu Tanzania(CHAWATA), John Mlaibu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na changamoto mbalimbali wanazozipata walemavu hasa katika usafiri hapa nchini na kuiomba serikali iwaangalie kwajicho la pekee, Kushoto ni mwasisi wa chama cha walemavu Tanzania(CHAWATA), Ali Piku.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwasikiliza viongozi wa chama cha walemavu Tanzania (CHAWATA) leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

CHAMA cha walemavu Tanzania(CHAWATA), kimeiomba serikali iboreshe upatikanaji wa huduma mhimu kwa watu wenye ulemavu ili kuwarahisishia maisha yao kwa kua itapunguza migongano inayojitokeza.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa chama cha walemavu(CHAWATA), John Mlaibu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa watu wenye ulemavu wengi wamekuwa hawapatiwi elimu,kunyanyapaliwa na umasikini ndio maana wengi wao wamebaki kuwa ombaomba.

Mlaibu ameiomba serikali kuwaangalia kwa jicho la pekee kwa kupunguza bei ya bajaji kwani si kila mlemavu anauwezo wa kununua bajaj ambayo itawasaidia kutembea na kufanya biashara ra usafirishaji mjini ikiwa wamekidhi vigezo vya kufanya biashara hiyo.

"Serikali iweke Ruzuku kwenye bajaj na vifaa vingine vinavyotumiwa na watu wenye ulemavu pekee ili kupunguza bei na watumiaji wamudu kuvinunua wenyewe" alisema Mlaibu.

Pia ameiomba serikali itangaze rasmi kuwa bajaj ziendeshwe na watu wenye ulemavu pekee na iwe moja ya ajira yao na watu wasio na ulemavu wowote wasitumie ili kuwasaidi watu hao.

Mlaibu ametoa wito kwa maderava  wote nchini hususani wa mabasi wawe waangalifu na kujali maisha yao na wengine na watii sheria za usalama barabarani ili kupunguza kasi ya ajali za kizembe ambazo zinasababisha ongezeko la watu wenye ulemavu kwani serikali imeshapambana na ugonjwa wa polio ambao ulikua kinara wa kusababisha ulemevu na sasa umetokomea kabisa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad