JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WAGONJWA WA KIPINDUPINDU KWA MIKOA YA ARUSHA NA MWANZA WAFIKIA 171

Share This
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
TAKWIMU za Ugonjwa wa Kipindupindu zinaonesha kupanda kwa mikoa ya Mwanza na Arusha kwa kuwa na wagonjwa 171, kutoka wagonjwa wa mwanzo 105.

Katika mkoani Arusha maambukizi yameongezeka kutoka wagonjwa 60 hadi kufikia wangonjwa 111 huku mkoa wa Mwanza maambukizi mapya kutoka wagonjwa 45 hadi 60.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla amesema kasi ya maambukizi ya ugonjwa kwa wiki iliyopita imepungua katika mikoa ya Mbeya na Tanga huku mikoa ya Dar es Salaam na Lindi ikiwa haina taarifa za maambukizi mapya ya wagonjwa wa kipindupindu.

Kigwangalla amesema kuwa katika mikoa ambayo haijakuwa na taarifa za wagonjwa wapya wa kipindupindu wizara imetaka wadau wa mikoa hiyo kuendelea kwa jitihada walizozifanya katika kudhibiti ugonjwa huo.

Kigwangala amesema ugonjwa wa kipindupindu tangu kuanza kulipotiwa hapa nchini watu 202 wamefariki dunia.

 Aidha amewataka madiwani na viongozi wa kisiasa kuhamasisha usafi wa mazingira na kushindwa kufanya hivyo wanahatarisha nafasi zao.

WAKATI HUOHUO.
Na Magret Kinabo wa Maelezo anaripoti.

SERIKALI imezitaka kila halimashauri nchini kuhakikisha kuwa inatenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya damu ili kuwezesha wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo kuipata na kuepusha kupoteza maisha ya watu hususan wakina mamawajazwazito na watu waliathirika na ajali.

Aidha Serikali imesema damu hutolewa bure, hivyo  mtu yoyote atakayeuziwa damu ataoe taarifa kwa Mkuu wa Mkoa,  Mkuu wa Wilaya  au wizarani ili wahusika waeze kuchukuliwa hatua. Hivyo Watanzania wasikubali kutoa rushwa kwa ajili ya kupata  damu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi  Kingwangala katika ziara aliyoifanya leo katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu  zilizopo jijini Dares Salaam.

Awali akitembelea ofisi hizo, Dkt Kingwangala  alielezwa na Dkt . Avelina Mgasa kwamba changamoto zilizopo katika upatikanaji wa damu nchini ni halimshauri kutenga bajeti za kutosha kwa ajili ya huduma hiyo.

“ Mganga Mkuu au Mkurugenzi ambaye hatawajibika kuhakikisha damu inakuwepo katika vituo vya kutolea huduma ataripotiwa kwa mamlaka zilizomteua ili ziweze kumchukulia hatua,” alisema Dkt. Kingwangala.

Dkt. Kingwangala aliitaka mifumo ya bima nchini kuhakikisha iligharamia mifuko ya kuhifadhi damu na reagent(vitenganishi) kwa wagonjwa waowalipia huduma za afya  ili kuweza kusiadi changamoto inayoikabili ofisi hiyo.

Aidha Dkt. Kingwangala aliitaka ofisi hiyo kuwa na mfumo wa kieletroniki wa kuwatambua watu wanaochangia damu, kutoa taarifa jinsi damu zao zilivyookoa miasha ya wagonjwa   na kuwapa motisha ili waweze kuwa wachangiaji endelevu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad