JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


TUME YA TAIFA YA TANZANIA UNESCO YAZINDUA HUDUMA MPYA YA NITAFUTEAPP

Share This
Na Zainabu Hamis,Globu ya Jamii.
TUME ya Taifa ya Tanzania UNESCO kupitia Dawati la Vijana imezindua huduma mpya ya Jamii iitwayo NitafuteApp.

Huduma hii inalenga kuwezesha Utafutaji,Utambuzi,Uokozi, Matibabu na Utoaji taarifa za watu waliopotea hususani Watoto,Wagonjwa wa Akili na Wahanga wa usafirishaji haramu wa binaadamu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo Afisa Mtendaji Mkuu wa Huduma hiyo Trayphone Elias amesema kuwa faida zinazopatikana katika mtandao huo ni Kukuza matumizi sahihi ya teknologia, kutoa huduma ambatanishi kwa kuunda timu maalum ya uokoaji na tiba za kisaikologia pamoja na Kuboresha usalama wa Kijamii,Kukuza matumizi ya lugha ya Kiswahili, Kukuza Uchumi wa Tanzania kwa kuliteyea Taifa fedha za kigeni na Kutengeneza zaidi ya ajira 3000 mnamo mwisho wa mwaka 2017.

Huduma hii itazinduliwa rasmi kiofisi Januari ,25 mwaka huu jijini Dar es salaam na inakusudia kuwaalika wadau na Washirika wa huduma ya NitafuteApp wakiwemo Tume ya Taifa UNESCO Tanzania,Tume ya Taifa ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania (TCRA),Wizara ya Mambo ya Ndani,Wizara ya Mambo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Makampuni ya Simu,NGO’S,Mashirika ya Misaada na wengine wengi.

Aidha Afisa Network wa NitafuteApp Shamte, Khamis amesema kuwa Huduma hii ni bure kabisa kwa watumiaji wote isipokua tozo kidogo kuanzia tarehe Machi,1,2016 kwa kila pachiko/tangazo jipya la anayehitaji huduma. 

Huduma hii imegaanyika katika makundi manne ikiwemo Taasisi za Kiselikali,Jumuiya,Vyombo vya Habari pamoja na Watumiaji wa nje ya Nchi.

NitafuteApp imefungua mifereji mbalimbali ya mawasiliano kwa wateja wake;Website ya Mradi (www.nitafuteapp.co.tz),Ukurasa wa facebook:NitafuteApp www.facebook.com/nitafuteapp,Akaunti ya Instagram: NitafuteApp www.instagram.com/nitafuteapp na Akaunti ya Twitter:NitafuteApp www.twitter.com/nitafuteapp. Kwa namba za simu Tembelea Tovuti ya www.nitafuteapp.co.tz/appinfo/our-app.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad