JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SINGITA GRUMETI YATOA MSAADA WA KOMPYUTA MAHAKAMA WILAYA YA SERENGETI.

Share This

Kutoka kushoto: Afisa tawala  katika mahakama ya Wilaya ya Serengeti Faraja Barakasi, Hakimu Makazi Mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Serengeti Ismael Ngaile,  Meneja Mahusiano wa Singita Grumeti Reserves na Grumeti  Fund  Ami Seki ,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Serengeti(DED) Naomi Nnko,  Katibu tawala wa Wilaya ya Serengeti(DAS) Cosmas Qamara,  Laurian Lamatus ,Moremi Mrigo na Samson Ndeki ambao wa wote ni wafanyakazi wa Grumeti wakiwa katika halfa ya kukabidhi msaada wa vifaa vya tehema vilivyotolewa na Grumeti kwa mahakama ya Wilaya ya Serengeti hivi karibuni

Na Anthony Mayunga.
Mahakama ya Wilaya ya Serengeti imepokea msaada wa vifaa vya kisasa vya tehama (ICT) ambavyo vimetolewa na kampuni ya utalii ya Singita Grumeti Reserves na shirika lake dada la Grumeti Fund.
Vifaa hivyo ikiwemo kompyuta na printa vilikabidhiwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Serengeti Ismael Ngaile katika hafla iliyofanyika katika ofisi za mahakama hiyo iliyopo mjini Mugumu.

 Ngaile alishukuru Grumeti kwa kuitikia ombi lao kuwapatia vifaa hivyo na kuahidi kuvitumia kuboresha huduma katika mahakama hiyo.

“Tulikuwa tunafanya kazi kwa kutumia computer moja lakini sasa ufanisi utaongezeka na nakala za hukumu zitatoka  mapema kuliko ilivyokuwa zamani. Hivyo kwakweli tunashukuru sana ”,alisema Ngaile.

Meneja wa Mahusiano wa Singita Grumeti Reserves  na Grumeti Fund  Ami Seki  alisema msaada huo ni sehemu tu  ya mchango wanaotoa kuboresha huduma mbalimbali kwa wananchi wa Wilaya za Serengeti na Bunda , Mkoani Mara.

  “ Tuna amini  kuwa vifaa hivi vitasaidia kurahisisha kazi za kiofisi na hivyo kuboresha huduma  na hii ni sehemu tu ya misaada inayotolewa na Singita Grumeti Reserves kwa kushirikiana na Grumeti Fund kuboresha huduma kwa wananchi”, alisema Seki.

Akizungumza katika halfa hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Serengeti (DAS) Cosmas Qamara alisema vifaa hivyo vitaiwezesha mahakama hiyo kufanya kazi kwa kutumia teknolojia ya kisasa na hivyo kuharakisha upatikanaji wa haki.

“Nina imani sasa wananchi watakuwa wanapata nakala za hukumu ndani ya wiki moja badala ya miezi mitatu  na ni hatua nzuri katika kupata haki kwa wakati”, DAS Qamara alisema.

Alitumia fursa hiyo kuishukuru Grumeti kwa kuendelea kutoa misaada mbalimbali ambayo inasadia kubadilisha maisha ya wananchi.

“Tunatadhamini sana juhudi mnazozifanya. Hii sio mara ya kwanza kupata msaada kutoka kwenu (Grumeti). Mmefanya mambo mengi mazuri katika sekta za elimu, maji na afya”, alisema Qamara.

Hafla hiyo pia ilihudhuria na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti (DED) Naomi Nnko na Mwenyekiti wa Halmashuri hiyo Juma Porini.

Viongozi hao pia walisema kampuni ya Grumeti imeonesha mfano ambao unapaswa kuigwa na wawekazaji wengine ambao wamewekeza katika wilaya hiyo.

“Grumeti ni wadau wetu  muhimu sana. Wamefanya mambo mengi sana na wadau wengine wajifunze kutoka kwao”, alisema Mwenyekiti wa Halmashauri ya Serengeti Juma Porini.

Singita Grumeti Reserves Ltd ni kampuni ya kitalii ambayo inaendesha hoteli kadhaa za kifahari katika mapori tengefu ya Grumeti na Ikorongo yaliyopo Mkoani Mara . Hoteli hizo zinamilikiwa na Paul Tudor Jones, ambaye ni mwekezaji kutoka Marekani.

Na Grumeti Fund ni shirika dada la Singita Grumeti Reserves Ltd ambalo linashugulikia uhifadhi wa maendeleo ya jamii.

Uwekezaji katika miradi ya jamii ambao unafanywa na Singita Grumeti Reserves kwa kushirikiana na Grumeti Fund unaripotiwa kupunguza vitendo vya uwindaji katika mapori tengefu ya Ikorongo na Grumeti.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad