Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya akisisitiza umuhimu wa kuwa na Kituo cha Afya chenye vifaa tiba, tarehe 12 Januari 2016, wakati alipokuwa akikagua ukarabati wa kituo cha Afya cha Chipole wilayani songea vijijini, baada ya kituo hicho kuungua mwaka 2013 na Ofisi hiyo kukikarabati. (wa kwanza kulia) ni Makamu wa Mama Mkubwa Chipole, Sista. Sairis Mkinga.
Daktari wa Kituo cha Afya cha Chipole, Ismail Mzimya akieleza umuhimu wa kituo hicho kwa wananchi wa Kata ya Magagura wilayani Songea vijijini wakati Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya tarehe 12 Januari 2016, alipokuwa akikagua ukarabati wa kituo hicho baada ya kituo hicho kuungua mwaka 2013 na Ofisi hiyo kukikarabati. (wa kwanza kulia) ni Makamu wa Mama Mkubwa Chipole, Sista. Sairis Mkinga.
Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya akiwa katika picha aya pamoja na Viongozi , watumishi na wananchi wanao hudumiwa na Kituo cha Afya Chipole wilayani songea vijijini tarehe, 12 Januari, 2016, baada ya kukagua ukarabati wa kituo hicho , kilichoungua mwaka 2013 na Ofisi hiyo kukikarabati.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Na. Mwandishi Maalum.
SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa imeahidi kukamilisha ukarabati wa Kituo cha Afya cha Chipole Songea Vijijini kilichopata majanga ya moto baada ya kituo hicho kuungua mwaka 2013 na Ofisi hiyo kutoa fedha za kukikarabati.
Akiongea wakati wa ziara ya kukagua ukarabati wa kituo hicho, tarehe 12 Januari, 2016, Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya amebainisha kuwa kufuatia kuungua kwa hospitali hiyo Ofisi ya Waziri Mkuu ilitoa kiasi cha shilingi milioni 35 kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho.
“Tumekagua ukarabati wa kituo hiki cha afya na tumeona pamoja na kuambiwa na uongozi wa hospitali hii kuwa pamoja na fedha tulizozitoa lakini bado kuna mahitaji ya msingi yanahitajika ili hospitali hii iweze kuwahudumia wanakijiji wanao izungunka hospitali hii. Tunaahidi kukamilisha ujenzi wa chumba cha kuhifadhi maiti pamoja na maabara” alisema Msuya.
Awali akitoa maelezo ya maendeleo ya ukarabati wa kituo hicho cha afya , Makamu wa Mama Mkubwa wa Chipole, Sairis Mkinga, alifafanua kuwa pamoja na mapungufu ya chumba cha maabara lakini bado kituo hicho cha afya kinao upungufu wa vyumba vya kuhudumia wagonjwa.
“Tunayo changamoto bado ya kuwa na sehemu maalum ya Mapokezi ya wagonjwa na wagonjwa kupokea dawa. Pia panahitajika mahali kwa akina mama wajawazito kujifungulia kwani kwa sasa vyumba hivi viko karibu sana na vyumba vya wanaume lakini tunahitaji chumba maalum kwa aijili ya kliniki ya watoto” alisisitiza Sista Mkinga.
Kituo cha Afya cha Chipole kilichopo Kata ya Magagura wilayani Songea vijijini kinamilikiwa na Shirika la watawa wa Mtakatifu Agnesi Chipole na inahudumia takribani wakazi 7,434 wa kata hiyo, hivyo kukamilika kwa Hospitali hiyo kutawezesha kupunguza vifo vya mama na motto pamoja na uboresha hali za afya za wakazi hao.
No comments:
Post a Comment