JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


NHIF YATAMBUA UMUHIMU WA WATOA HUDUMA ZA AFYA.

Share This
Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeipongeza Manispaa ya Ilala kwa kutoa huduma bora za afya kwa wanachama wa mfuko huo.

Akizungumza na waandishi wa habari, katika ufunguzi wa mkutano wa watoa huduma wa afya uliofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Masoko,Elimu kwa Umma na Utafiti Othuman Rehani (Pichani)amesema kwamba Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unatambua mchango mkubwa unaotolewa na watoa huduma za afya kwa wanachama wao.

“Utoaji wetu wa huduma za afya za kijamii kwa wanachama wetu umekua ukitegemea Hospitali za Umma na Binafsi”alisema Rehani.

Mkurugenzi Othuman Rehani aliongeza kuwa NHIF wanaamini kwamba, ushirikiano na watoa huduma utasaidia Serikali yetu ya awamu ya tano kufikia lengo lake la kutoa huduma bora.

Aidha Rehani ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa Bima ya Afya mwaka 2001 yakiwemo; kupanuka kwa upatikanaji wa huduma kwa kuongezeka kwa vituo vya kutolea tiba vilivyosajiliwa na mfuko,usajili wa maduka ya dawa yalioongeza upatikanaji wa dawa hadi vijijini,utoaji wa mikopo ya madawa na vifaa tiba ili kuimarisha utoaji wa huduma za afya pia kuongezwa kwa vitita vya mafao kwa wanufaika waliokua wakiongezeka mwaka hadi mwaka.

Katika mkutano huo wadau mbalimbali wa afya waliohudhuria ni pamoja na Mganga Mkuu wa Wilaya,Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Meneja Mfawidhi wa Mkoa wa Ilala na Wakurugenzi wa Hospital za Rufaa.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umetimiza miaka 14 toka ulipoanzishwa na kuanza utekelezaji wake mwaka 2001 ikiwa na watoa huduma za afya wale wa hospitali za Umma na Binafsi waliokamilisha usajili wao katika Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Wazee na Watoto.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad