JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA(TEA) YAWEZESHA AWAMU YA PILI YA MAFUNZO WEZESHI KWA WALIMU (STEP)

Share This
Walimu (Msingi) wakishiriki mafunzo ya Kujenga Uwezo katika ufundishaji na ujifunzaji katika Mkoa wa Ruvuma. Mafunzo hayo yanawezeshwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

MAMLAKA ya Elimu Tanzania kwa kushirikiana na  Wizara ya Elimu, Sayansi, na Teknolojia, na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imewezesha awamu ya pili ya Programu ya kujenga uwezo wa walimu na wanafunzi, kwa walimu mahiri (Msingi) wa masomo ya Hisabati, Kiswahili na Kiingereza  katika mikoa mitatu nchini; Songea, Katavi, na Singida.

Lengo la mafunzo haya ni kuwawezesha walimu kuwatambua wanafunzi wenye uwezo mdogo kimasomo na kuwapatia mafunzo rekebishi; na kuwajengea uwezo ili wote wawe na uelewa unaolingana.

Programu ya kujenga uwezo wa walimu na wanafunzi katika ufundishaji na ujifunzaji (Student Teaches Enrichment Program)  ni moja kati ya mikakati  9 iliyoibuliwa wakati wa maabara ya BRN katika sekta ya elimu ambao unatekelezwa kupitia mafunzo kwa walimu, na kufadhiliwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania.

Awamu ya kwanza ya mafunzo haya ilihusisha  Halmashauri 40 ambapo jumla ya walimu 19,300 walipatiwa mafunzo kwa mwaka 2014/15. Hii ni awamu ya pili ya mafunzo haya ikihusisha halmashuri 60 ambapo jumla ya walimu mahiri 900 wanawezeshwa katika vituo 8 vilivyoteuliwa kuwa mwenyeji wa mafunzo haya, yanayolenga kuwafikia walimu 18,501 katika mwaka huu wa fedha 2015/2016.

Mafunzo wezeshi kwa walimu wa sekondari wa masomo ya Kiingereza, Hisabati, Kiswahili, na Biology nayo yanaendelea kwa ufadhili wa Mamlaka ya Elimu Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad