JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA YAONGEZEKA TANZANIA

Share This
Mtaalamu wa masuala ya Afya kutoka akipima mzunguko wa damu Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukizwa (TANCDA)jana katika hospitali ya mkoa wa Mount Meru ambapo shughuli za upimaji wa magonjwa ya moyo,kisukari na saratani yalifanyika bure kwa wananchi wote.
Wakazi wa Arusha wakiwasikiliza waelimishaji wa magonjwa yasiyoambukiza kutoka Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukizwa (TANCDA)jana katika hospitali ya mkoa wa Mount Meru ambapo shughuli za upimaji wa magonjwa ya moyo,kisukari na saratani yalifanyika bure kwa wananchi wote.

Na Woinde Shizza,Arusha.
Kutokana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo magonjwa ya moyo ,kisukari na saratani ,Watanzania wameaswa kuzingatia lishe bora na mtindo bora wa maisha ili kuepuka magonjwa hayo ambayo husababishwa na mtindo mbaya wa maisha pamoja unywaji pombe,uvutaji sigara na ulaji uisiofaa.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukizwa (TANCDA) ,Dokta Tatizo Waane alisema kuwa kumekua na ongezeko kubwa la watu wenye magonjwa hao kitaifa ambapo ugonjwa wa moyo asilimia 26% ugonjwa wa kisukari umeongezeka kwa Asilimia 9.6.

Akizungumza katika zoezi la upimaji na utoaji elimu kwa wananchi juu ya magonjwa hayo ,Dr.Waane amesema kuwa magonjwa ya moyo yameongezeka kwa asilimia 10 hivyo Watanzania hawana budi kuangalia hali yao ya lishe na kuzingatia kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima.

"Watu wengi wamekua hawatilii maanani magonjwa yasiyoambukiza lakini yana athari kubwa kiafya na kwenye uchumi wa watu kwani hutumia muda mrefu na fedha nyingi kutibu" Alisema Dokta Waane.

Mratibu wa zoezi la upimaji wa magonjwa hayo kwa mkoa wa Arusha Dokta David Shungu alisema kuwa wananchi wanapaswa kupatiwa elimu kwani magonjwa hayo yanaongoza kwa kusababisha vifo sawa na magonjwa yanayoambukiza.

Kwa upande wake Mkazi wa Arusha aliyejitokeza kupima afya yake na kupata ushauri Tunu Ndege alisema kuwa zoezi hilo litawasaidia wananchi wengi kujua afya zao na kuchukua hatua kulinda afya zao dhidi ya magonjwa ,pia ameshauri huduma hiyo ya upimaji iwafikie watu wa vijijini wanaoteseka na magonjwa bila kujua.


Alisema Mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza ya moyo,sukari na saratani yanapaswa kutiliwa mkazo kwa kutoa elimu na tiba kwa wananchi kwani magonjwa hayo hudumu kwa muda mrefu na kusababisha hasara ya kijamii na kiuchumi hata kupelekea vifo na ulemavu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad