Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Ummy Mwalimu na Kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea, Damian Dallu.
Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kupongeza jopo la
Madaktari waliomhudumia katika Hospitali ya Mhimbili.
Katika mkutano huo Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alitoa zawadi za kadi za pongezi kwa baadhi ya madaktari mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Ummy Mwalimu akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Mhimbili, Profesa Mohamed Janabi.
Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akiingia
katika ukumbi wa mikutano katika kitengo cha Moyo cha Taasisi ya Jakaya
Mrisho Kikwete kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee Mhe Ummy Mwalimu akimkaribisha Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ili aweze kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Kulia
ni aliyekuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwashamu
Askofu Titus Mdoe na Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea, Damian Dallu wakiwa
katika mkutano wa Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama
Polycarp Kardinali Pengo na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mkutano
wa Kitengo cha Moyo cha Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo katika Hospitali
ya Taifa ya Mhimbili.
Katibu Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Dkt. Mpoki Ulisobisya akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na swali lililoulizwa na mwandhishi wa habari kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee haitoi ruhusa ya mtu yoyote kwenda kutibiwa nje ya nchi na ruhusa hiyo hutolewa na Madaktari wenyewe ambao walikua wanamtibia mgonjwa.
Na Chalila Kibuda
wa Globu ya Jamii.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amepongeza weledi wa huduma za
madaktari na huduma zinazotolewa katika Tasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es
salaam.
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ametoa pongezi hizo jana
Ijumaa Januari 8, 2016 wakati akizungumza na waandishi wa habari
hospitalini hapo ambako alikuwa amelazwa kwa uchunguzi wa afya yake na
matibabu.
Alisema
kwamba awali yeye alikuwa anaogopa kutibiwa hapo kutokana na taarifa
potofu zilizokuwa zinazotolewa kwenye vyombo vya habari juu ya
operesheni tata zilizowahi kufanyika katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, na kwamba sasa ameridhika kuwa ni vinginevyo kwani Kitengo
cha magonjwa ya moyo cha hospitali hiyo kimemdhihirishia kwamba kina
uwezo mkubwa wa matibabu ya moyo kama ilivyo hospitali zingine popote
pale duniani.
Askofu Mkuu huyo wa Jimbo kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alilazwa
katika taasisi hiyo ya moyo tangu Januari Mosi mwaka huu. Hali yake
imeendelea kuimarika kila siku baada ya kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa
matibabu hapo.
Kwa
upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na
Wazee, Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imeokoa kiasi cha
shilingi bilioni nne ambazo zilikua zipotee kwa ajili ya kupeleka
wagonjwa wa moyo kutibiwa nje ya nchi.
Aidha Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo
katika hospitali ya Taifa ya Mhimbili, Profesa Mohamed Janabi amesma
kuwa Askofu Pengo ataruhusiwa mwisho wa juma hili kwa kuwa afya yake
imeimarika.
No comments:
Post a Comment