JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


YAMOTO BENDI WAINGIA TUZO ZA KORA

Share This
Waimbaji wa yamoto bendi wakiwa katika picha ya pamoja.

Na Mwandishi Mwetu
WAKATI jana wakiendelea kutoa burudani katika mji wa Washington DC, Bendi ya Yamoto, imeingia katika kuwania tuzo za Kora 2016, ikiingia katika kipengele cha Most Promising Male Artist Of Africa.

Mkurugenzi wa bendi hiyo Said Fella, alisema kwanza anamshukuru Mungu vijana wake juzi usiku walikuwa na onesho lao la pili lililofanyika Washington DC na kuweza kufanya vizuri, lakini la pili kuingia katik tuzo za Kora. 

Fella ambaye ni diwani wa Kata ya Kilungule alisema ni kitu kikubwa sana kwake kwa bendi yake kuingia katika tuzo za Kimataifa.

Alisema kuingiaa kwa vijana wake katika tuzo hizo ni kitu kikubwa sana na kinazidi kuipandisha bendi yake ambayo sasa ipo nchini Marekani kwa ziara ya maonesho maalum.

"Ni kitu kikubwa sana kinazidi kutupandisha kutoka sehemu moja kwenda kwingine, tunaamini mwenyezi Mungu atatusimamia tuweze kupata kwa mashabiki wetu kuliona hili na kutuunga mkono katika kupiga kura"alisema Fella. 

Kwa upande wa ziara ya bendi yake nchini Marekani alisema vijana hao watafanya onesho la mwisho Desemba 12, katika mji wa Houston na baadae kurejea nchini kwa kazi zao nyingine. 

Alisema katika onesho la juzi walifanya onesho zuri la aina yake na katika mji wa Washington na kuudhuliwa na mashabiki wengi wa muziki. 

"Onesho letu la juzi lilikuwa zuri sana na limezidi kuongeza hamasa kwa vijana wazidi kujituma na kufanya viuri zaidi katika kuhakikisha wanapata mihaliko kama hii ya kuja nchini kama hizi ambazo nazo tumekuwa na mashabiki wetu"alisema Fella.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad