JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WENYEVITI WA CCM MIKOA WAPONGEZA RAIS DK. JOHN MAGUFULI KWA KASI YAKE

Share This
 Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ramadhan Madabida akizungumza na waandishi wa habari (hayupo pichani) juu ya kazi inayofanywa na Rais Dk. John Magufuli leo jijini Dar es Salaam.
 Waandishi wa habari wakimfatilia Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,Ramadhan Madabida leo jijni Dar es Salaam

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WENYEVITI wa Mikoa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamesema kuwa kasi ya Rais Dk. John Joseph Pombe Magufuli kwa kuwachukulia hatua watendaji wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao, wanapongeza kwa kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ,Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Wawenyeviti wa Mikoa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida amesema kuwa wenyeviti wanapongeza kwa hatua hizo ambazo amezifanya Rais Dk. John Magufuli.

Amesema watu walikuwa wanatoa huduma isiyo bora kwa wananchi hivyo kila mtu kwa nafasi yake afanye kazi yake kwa mujibu wa sharia

Madabida amesema kwa kasi hiyo wako tayari na maamzi yeyote ambayo anaweza kuyatoa kwa viongozi wa CCM ambao hawakuweza kufuata utaratibu.

Aidha amesema wananchi waunge juhudi ambazo Rais John Joseph Magufuli anafanya katika kuweza kila mtu aweze kuwajibika ipasavyo kuwahudumia wananchi wake.


Ameongeza kuwa Wenyeviti wataendelea kuwa pamoja na Rais katika majumu yake ya kuhakikisha nchi inakuwa na watendaji wanaojituma na kila nyakati ina dhana yake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad