JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WATU 493 WAMEFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIPINDUPINDU HAPA NCHINI

Share This
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na ugonjwa wa Kipindupindu ulivyoweza kupungua ikiwa kukiwa na vifo vya watu 493 kwa Tanzania Bara.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

Na Zainabu Hamis wa Globu ya Jamii.
JUMLA ya watu 493 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa kipindupindu Tanzania bara tokea ulipoibuka jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake leo, amesema kuwa jumla ya watu 12,222 wameugua ugonjwa huo tangu ugonjwa huo wa mlipuko kuaza hapa nchini.



“Ugonjwa wa Kipindupindu umeanza tokea tarehe Desemba 15, 2015 katika mkoa wa Dar es salaam na kusambaa katika mikoa 21 ya Tanzania” Mhe. Mwalimu amesema.



Hata hivyo,Waziri huyo,amesema waathirika wa kipindupindu wameanza kupungua katika mikoa ya 
Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es salaam.

Pia ameitaja Iringa na Kilimanjaro kuwa ni mikoa ambayo imeweza kuthibiti ugonjwa huo hatari.

Mwalimu akitoa takwimu za ugonjwa huo, amesema hivi sasa kuna wagonjwa wapya 76, hivyo idadi ya wagonjwa wapya imefikia 493 na kifo kimoja.

“Hadi sasa mkoa wa Morogoro vijijini unaongoza kwa wagonjwa 56, ukifuatiwa na Arusha (28), Rorya (22), Bunda (21) na Kigoma vijijini 17.” Mhe. Mwalimu amesema”

Aidha Mhe.Mwalimu ametoa agizo kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuwa ni marufuku kuuza matunda yaliyokatwa barabarani,kuuza vyakula katika mazingira yasiyo safi na salama,huku akitaka kuandaliwa kwa taarifa za kila wiki kuhusu ugonjwa huo.

Akitoa rai kwa wakuu wa wilaya na mikoa, kuwa walete taarifa sahihi za mlipuko wa ugonjwa huo kwa ajili ya kuudhibiti. Na kwa kuwasisitiza watanzania kunywa maji safi na salama na kunawa mikono kwa maji safi na salama.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad