JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LACHANGISHA DIRHAM MILIONI MOJA KWA AJILI YA “WE CARE"

Share This
 Shirika la ndege likiwatunuku timu ya soka kutoka Serbia kama bingwa wa michuano ya kombe la dunia la mashirika ya ndege upande wa soka.
 Bendi ya vijana wenye ulemavu wa kusikia kutoka taifa la Falme za kiarabu wakiimba wimbo wa taifa la Falme za Kiarabu.
  Afisa mkuu wa biasaha wa Shirika la Etihad, Peter Baumgartner, akitumbuiza wakati wa tamsha.
 Dr Khawla Salem Al Saaedi, mwakilishi wa Rais wa shirika la kimataifa la umoja wa wanawake na afya, akiwazawadia timu kutoka Nepal kwa kushinda michuano ya kimataifa ya mavazi.

 Kamati ya Michezo na Jamii wakiwa na baadhi ya wahiriki wa michuano ya kimataifa ya mavazi.
 Kamati ya Michezo na Jamii wakiwa na baadhi ya wachezaji wa soka.
Abu Dhabi-based Fusion Arts ballet wakitoa burudani wakati wa tamasha. 

SHIRIKA la ndege la Etihad, ndege rasmi ya taifa za Falme za kiarabu, imefanikiwa kuchangisha kiasi cha dirhams milioni moja kwa ajili ya kusaidia kampeni ya “we care Yemen” hii ikiwa ni pamoja na kusaidia kukarabati shule mbili nchini Kenya kama sehemu ya mpango wa kila mwaka wa shirika hili la ndege la kuchangisha fedha kwa kushirikiana na shirika la Red Crescent kutoka nchi ya Falme za kiarabu pia. 

Mchango huu ulitangazwa wakati wa kufunga sherehe za kombe la dunia la mashirika ya ndege kwa upande wa mpira wa miguu na tamasha la vyakula na fashion, vyote vikiwa vimeandaliwa na kamati ya michezo na jamii ya shirika la Etihad, lilofanyika ukumbi wa kimataifa wa Al Forsan. 

Timu za soka kutoka mashirika 28 ya anga na ndege yalishiriki kwenye tamasha hilo lilokuwa na mashindano mbalimbali yakiwemo uchoraji wa henna, burudani ya mziki, ballet and michuano ya mavazi. Shirika la Etihad lilitoa zawadi kemkem ikiwepo safari kwenda kenya kwa mshindi wakwanza na wapili.

Makamu wa raisi wa shirika la Etihad masuala ya siasa za anga, Khaled Al Mehairbi, anayetumikia kama mwenyekiti wa kamati ya michezo na jamii, alisema “ Kama shirika la ndege la taifa ya Falme za kiarabu, tunapenda kuthibitisha dhamira yetu kwa jamii na kujitolea kwa wale wenye uhitaji. Tunayo furaha kushirikiana na UAE Red Crescent katika kutumikia and kusaidia jamii husika”.

“Tungependa kutoa shukrani za dhati pia kwa wageni, wadhamini and wauzaji walioshiriki kwa mioyo yao ya dhati kuchangia kampeni hii kwa mwaka 2015 ili kusaidia wale wenye uhitaji. Kwa pamoja tumetoa mwanga wa matumaini na nafasi ya maisha bora ya baadae kwa kaka na dada zetu waliopo Yemen na Kenya”

Sherehe za ufunguzi ziliongozwa na bendi ya taifa ya vijana wasio na uwezo wa kusikia. Tamasha hilo lilishuhudia burudani kutoka kwa “Sala the Entertainer”, mshindi wa mashindano ya X Factor 2015, na msanii kutoka Marekani, Dynasty. Burudani kutoka kikundi cha watoto waliocheza “Ballet” pia ilikuwa kivutio kikubwa katika tamasha hilo.

Michango ya hisani kwa Yemen ilikusanywa kupitia matukio mbalimbali ikiwemo mchango wa “Etihad gGuest Miles Online”, Kupitia timu ya soka ya Etihad, Mauzo ya vitu kutoka Etihad, mchango wa vifaa vya shule na mabegi mapya kwenda kwa watoto nchini Yemen kupitia wafanyakazi wa shirika la ndege la Etihad, na mchango wa fedha taslimu kwenye visanduku vya Emirates Red Crescent.

Mipango ya shirika kusaidia kampeni ya “We Care Yemen” na Kenya ni sehemu ya makubaliano ya awali juu ya ushirikiano wa kiubinadamu na kijamii baina ya shirika la ndege la Etihad na Emirates Red Crescent.

Tukio hili la kijamii lilihudhuriwa na mheshimiwa Khadija Issa Yusuf, Balozi wa kenya kwa nchi ya Falme za kiarabu, Bw. Humaid R Al-Shamsi, Naibu katibu mkuu kwa misaada ya kimataifa kutoka shirika la Emirates Red Crescent, Dr. Khalwa Salem Al Saaedi, mwakilishi wa Rais wa shirika la kimataifa la muungano wanawake na afya.

Wengine waliohuduria walikuwa katibu mkuu, Mheshimiwa Mariam Saif Al Qubasi, Mkuu wa sekta ya mahitaji maalumu kutoka Zayed Higher Organization (ZHO), Hamad Alhosani, Mtendaji mkuu wa TCA Abu Dhabi, na Mohammad Ali Khilji, meneja mkuu wa Axiom UAE. 

Shirika la ndege la Etihad liliwakilishwa na Peter Baumgartner, Afisa mkuu wa biashara, Khaled Al Mehairbi, Makamu wa Rais masuala ya siasa za anga, Ali Al Shamsi, Makamu wa Rais Abu Dhabi Hub, Oliver Iffert, Makamu wa rais uendeshaji masuala ya Ndege, na Geert Boven, Makamu wa Rais huduma wa Uwanja wa ndege.

Mwaka 2015, shirika la ndege la Etihad liliweza kuchangisha Etihad Guest miles, bidhaa za msaada na fedha taslimu yenye thamani ya zaidi ya dirhams milioni tatu.

Tamasha hili la siku mbili lilifanyika kwa kushirikiana na Emirates Red Crescent, baraza la michezo la Abu Dhabi, vyombo vya habari vya Abu Dhabi, ukumbi wa kimataifa wa michezo wa Al Forsan, Hoteli za Time, Shirika la wanawake la Joyful, kampuni ya maji ya Al Ain, Bottega Verde, Dusit Thani Abu Dhabi, Axiom UAE, Sebamed, Fusion Arts, Gabs, Pierre Fabre, Hoteli za Yas Viceroy, Novotel Al Bustan, Holiday Inn Abu Dhabi, Hoteli za One to One, Yas Waterworld, Maabara za dawa za Al Borg Medical, Al Jaber Optical, Mikura Pearls, Conrad Dubai, Absolute Dry, Zartux, and Hoteli ya Tilal Liwa.


Kuhusu Shirika la Ndege la Etihad
Shirika la Ndege la Etihad lilianza shughuli zake mnamo mwaka 2003 na hadi kufikia mwaka 2014, ilikuwa limeshabeba abiria takriban milioni 14.8. Kutoka makao makuu yake huko Abu Dhabi, shirika hili linasafiri au limetangaza mipango ya kuhudumia wasafiri na mizigo kutoka vituo 116 huko Mahariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na nchi za Americas. Shirika lina ndege aina ya Airbus na Boeing takriban 120, Zaidi ya ndege 200 zikiwa zimewekea oda, zikiwemo Boeing 787s 66, Boeing 777Xs 25, Airbus A350s 62 na Airbus A380s tano.

Shirika la Etihad pia limewekeza katkia AirBerlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways , Virgin Australia, pamoja na shirika lenye makazi Uswiss Darwin Airline, likifanya biashara kama Etihad Regional. Shirika la Ethihad, sambamba na airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Etihad Regional, Jet Airways na NIKI, pia hushiriki pamoja nkwatika washirika wa Etihad Airways, brand mpya inayowaleta kwa pamoja mashirika mengine ya ndege yenye uelewa sawa ili kutoa huduma bora zaidi kwa wateja, kuwapa wateja ratiba nzuri Zaidi na kuwazawadia wateja wakudumu.kwa maelezo Zaidi, tafadhali tembelea :www.etihad.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad