JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
31/12/2015
TAARIFA YA JESHI LA POLISI
KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU TAHADHARI KATIKA
MKESHA WA MWAKA MPYA
Tunapoelekea kumaliza mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2016, wananchi hutumia muda huo kwenda katika nyumba za ibada ama kusherekea katika
maeneo mbalimbali ya starehe, ambapo uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya watu
hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vinavyohatarisha usalama wa raia mali zao.
Jeshi la Polisi nchini, limejipanga vizuri katika mikoa yote kwa
kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha kwamba
vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyojitokeza hususani katika kipindi hiki cha kuelekea
mkesha wa mwaka mpya vinadhibitiwa. Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya
kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote ambayo
yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.
Aidha, Jeshi la Polisi linatoa
tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na kuchukua hatua stahiki za haraka kwa
kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo yao
ya makazi ama maeneo ya biashara. Simu za polisi endapo mwananchi atakuwa na
taarifa ni 111 au 112.
Pia,
Jeshi la Polisi linawatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia
barabara kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa
madereva wa magari na pikipiki, kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kwenda mwendo
kasi, kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.
Vilevile, wananchi kuacha tabia ya kuchoma matairi barabani pamoja na
kupiga mafataki. Aidha, yeyote atakayefanya vitendo hivyo hatua kali za
kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Nawatakieni watanzania wote kheri ya mwaka
mpya.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya
Polisi.
No comments:
Post a Comment