JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


IGWUTA WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KAZI ZAKE

Share This
Na Zainabu Hamis wa Globu ya Jami.
CHAMA cha wafanyakazi wa viwanda na sekta mbalimbali(IGWUTA) champongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Joseph Magufuli (Pichani)kwa namna na jinsi anavyofanya kazi yake hasa ile ya kupambana na mafisadi na wanafiki.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Katibu Mkuu wa chama chama cha IGWUTA, Michael Kashamba amesema kuwa,Wamefurahishwa kwa  kumpata Rais Magufuli na wanatoa wito kwa Wafanyakazi wote hapa nchini kujitokeza na kumuunga mkono Rais wetu katika mapambano dhidi ya ufisadi.

Aidha Kashamba ametoa tamko la kumpongeza Magufuli kuwa ni kiongozi asiyekuwa wa kawaida, Hana ubinafsi na anaweka maslahi ya nchi mbele huku akimfananisha kwa utendaji wa kazi zake ni kama Rais wa awamu ya kwanza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Pia Kashamba amesema kuwa, Chama chao kinatoa huduma ya kuelimisha na kuhamasisha wanachama kutimiza wajibu wao wa kufanya kazi kwa bidii, nidhamu na uaminifu mkubwa.

Pia IGWUTA inatoa Huduma za utetezi kwa Wanachama dhidi ya uonevu wowote uliofanywa na baadhi ya waajiri hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad