JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII WATOA TAARIFA YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU

Share This
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Donan Mmbando akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya Mlipuko wa Ugonjwa wa kipindupindu uliopo sasa ulianza mnamo 15 Agosti 2015, katika Manispaa ya Kinondoni na baadae kusambaa katika Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam leo jijini Dar es Salaam.
  Waandishi  wa habari wakimsikiliza  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Donan Mmbando, leo jijini Dar es Salaam
Wadau mbalimbali wakiwa katika mkutano huo leo  jijini Dar es Salaam
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MLIPUKO wa Ugonjwa wa kipindupindu umesambaa katika mikoa 14  na kufikia wagonjwa 7825 na vifo 106.

Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Donan Mmbando amesema kati ya wagonjwa wote waliougua 3746 sawa na asilimia 67 wanatoka katika mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema kuwa  Mikoa inayotoa taarifa ya kuwepo wagonjwa wapya ni Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Dodoma, Mwanza, Arusha, Mara, Singida na Tanga.

 Mmbando amesema kuwa  ugonjwa huo umeripotiwa katika mikoa mingine ya Tanzania ikiwa ni pamoja na Pwani, Singida, Mara, Arusha, Tanga, Mwanza, Shinyanga, Morogoro, Iringa, Kilimanjaro, Dodoma, Kigoma, Geita pamoja na Rukwa.

Aidha amesema hadi kufikia Novemba 8,2015  idadi ya wagonjwa waliokwisha kuripotiwa tangu mlipuko uanze hapa nchini ni 7825 na vifo 106 amabo ni asilimia 1.3 ya waliougua.

Amesema hatua walizozichukua kwa ugonjwa huo ni kutoa dawa, vifaa vya maabara na vifaa kinga kwa mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro.

Aliongeza kuwa  Wizara imepokea maombi kutoka mikoa ya Singida, Arusha, Tanga, Mwanza, Mara na Geita kati ya Oktoba 15 mwaka huu  na yanashughukuliwa na utawala, Kupima vipimo vya maabara na kufuatilia ubora wa vipimo kutoka katika mikoa iliyofanya uchunguzi na kuthibitisha uwepo wa ugonjwa huo, Kupeleka timu za watalaam kutoka ngazi ya Mkoa na Taifa kusaidiana na timu za Wilaya husika. 

Aidha tarehe 28 Oktoba 2015, Timu ya Kitaifa ilienda katika mikoa ya Tanga, na Singida na vilevile mkoa wa Manyara pia timu ilienda kwa ajili ya kufuatilia tarifa za kuwepo kwa ugonjwa wa kuhara na kutapika – taarifa ya timu hizi inakamilishwa na itawasilishwa.

Mmbando amesema hatua nyingine Kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya juu ya ufuatiliaji wa ugonjwa na utoaji wa matibabu ,Kutoa elimu ya kwa umma kupitia vyombo vya habari hususani radio na runinga. Aidha, mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini yametolewa, Kuandaa “Water safety plan” kwa kushirikisha wadau mbalimbali ikiwemo WHO, PSI, CDC, MSF, Redcross na USAID. Aidha mpango mkatati huu utajikita kwanza kwa jiji la Dar es salaam kwa kuanzia na hapo baadae itaenda katika mikoa mingine.

Amesema changamoto katika ugonjwa huo ni,Mwitikio hafifu wa jamii juu ya kukabiliana na ugonjwa huu,Jamii kutokuzingatia kanuni za afya na mazingira,Ushiriki mdogo wa sekta nyingine katika kupambana na ugonjwa huu,Ukosefu wa pesa za kuwalipa watumishi wa afya wanaohusika katika zoezi la kukabiliana na ugonjwa huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad