Mkuu wa kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa na Kaimu mkuu wa kitengo cha Masoko benki ya Barclays, Joe Bendera wakiwa wameshika picha ya kombe la mpira ambayo litatembezwa Disemba 3 na 4 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwaajili ya wapenzi wa mpira wa miguu kupiga nalo picha ikiwa mwaka huu benki ya Barclays ni mwisho wa kudhamini ligi kuu uingereza.
Kaimu Mkuu wa kitengo cha Masoko benki ya Barclays, Joe Bendera akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na benki hiyo kutembeza kombe la Barclays premier ligi ya Uingereza kulitemeza jijini Dar es Salaam kwaajili ya wapezi wa soka jijini hapa kupiga nalo picha ambazo itakuwa kumukumbu kwao.Kusoto ni Grace Josef na kulia ni Rhobina Justine wakiwa ni miongoni wa washiriki wa benki hiyo katika kutembeza kombe hilo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa akizungumza na waandishi wa habari kuhuriana na ratiba ya kombe hilo litakavyokuwa likizungushwa ili wapenzi wa soka kupiga picha na kombe ikiwa benki ya Barclays ni mwaka wa mwisho kudhamini ligi ya Uingereza.
BENKI ya Barclays hapa nchini inatarajia kuwaletea
wapenzi wa soka kombe la ligi kuu ya Uingereza kwa ajili ya kupiga nalo
picha ikiwa mwaka huu ni mwisho wa benki hiyo kudhamini ligi kuu nchini
Uingereaza, Pia wananchi wameombwa kujitokeze kufungua akaunti kwa
ajili ya mshara katika benki hiyo ili kujishindia tiketi mbili za kwenda
kuangalia ligi kuu ya Uingereza.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar,Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Masoko benki ya Barclays, Joe Bendera alifafanua
kuwa "Wapenzi wa soka wajitokeze kwa mujibu wa ratiba ya benki a
Barclays kwaajili ya kugipatia picha wakiwa na kombe la benki hiyo ikiwa
ni mwaka huu ni wa mwisho kudhamini ligi kuu ya Uingereza iliyokuwa
ikijulikana kama Barclays Premier League." Bendera
Nae Mkuu
wa kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa amesema
kuwa Disemba 3 mwaka huu kombe hilo litaanzia katika tawi kuu la benki
benki hiyo Posta kuelekea Mwembe yanga kupitia
barabara ya Pungu mpaka Temeke Hospitali, Uwanja wa Taifa, kituo cha
magari cha Mombasa na kumalizia viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es
Salaam.
Na
Disemba 4 litaanzia kutembezwa kutokea katika benki ya Barclays tawi la
Alpha kuelekea ofisi za IPP Media, Mlimani City, tawi la benki hiyo la
Slip way Kinondoni Biafra, Mazese Darajani na kuishia katika viwanja vya
Karume jijini Dar es Salaam.
Aidha Mwakyusa
aliyoa wito kwa wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kupiga
picha na kombe la ligi kuu ya Uingereza ambapo mwaka huu ni mwisho wa
benki ya Barclays kudhamini ligi kuu Uingereza.
No comments:
Post a Comment