Taasisi
ya Benjamin William Mkapa inasikitika kuwatangazia Umma kwamba kumekuwa
na udanganyifu au utapeli unaoendeshwa na baadhi ya watu wasiojulikana
wakitumia jina la Taasisi hii katika kutoza fedha watu mbalimbali
wakidai kusaidia kupata ajira au ufadhili wa masomo katika sekta ya
afya.
Baadhi
ya wadanganyifu hao wamekuwa wakitumia barua au akaunti yenye jina
“Benjamini Mkapa” katika mtandao wa kijamii wa ‘facebook’ ambapo
huwasiliana na watu, na kuwahadaa kuwa watawapatia ajira au ufadhili
baada ya kujaza fomu na kutoa fedha katika mchakato mzima.
Taasisi
ya Benjamin William Mkapa (ijulikanayo kama “Benjamin W. Mkapa HIV/AIDS
Foundation”) inapenda kuwatangazia umma kuwa haihusiki na utaratibu huo
wa udanganyifu au utapeli. Tunapenda kuwasisitizia wananchi kwamba
hakuna fedha yoyote inayotozwa na Taasisi kwa ajili ya kupata ajira au
ufadhili wa masomo chini ya miradi inayoendeshwa na Taasisi yetu.
Kwa
mtu yoyote mwenye kutaka kupata habari za uhakika na kamili juu ya
masuala hayo, tafadhali, awasiliane na ofisi ya makao makuu iliyopo Dar
Es Salaam, na ofisi za Kanda zilizopo Mwanza, Mtwara na Iringa, au kwa
kupitia email: info@mkapahivfoundation.org au facebook account: www.facebook.com/BenjaminWilliamMkapaHivAidsFoundation, namba za simu +255 22 2618556-9
Taasisi
kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wanaendelea na uchunguzi ili
kuwabaini na hatimaye kuwatia kwenye mikono ya sheria wadanganyifu hao.
Imetolewa na:
Menejimenti ya Taasisi ya Benjamin William Mkapa
No comments:
Post a Comment