jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA

Share This
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.

       TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI.
   “PRESS RELEASE” TAREHE 24.11.2015.
MWENDESHA PIKIPIKI AUAWA KWA KUCHOMWA KISU NA KISHA KUPORWA PIKIPIKI YAKE.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA SILAHA KINYUME CHA SHERIA.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MWENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA MKAZI WA MWAKA KATIKA MJI MDOGO WA TUNDUMA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JOHN SIMWITO KABUJE [22] AUAWA KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI UPANDE WA KUSHOTO NA KISHA  KUNYANG’ANYWA PIKIPIKI AMBAYO BADO KUFAHAMIKA NAMBA ZA USAJILI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 23.11.2015 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO MTAA WA MAPOROMOKO, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. 

INADAIWA KUWA, MAREHEMU AKIWA NA KATIKA KAZI YAKE, ALIKODIWA NA MTU MMOJA NA WAKATI WAKIWA NJIANI WALIJITOKEZA WATU WENGINE WATATU AMBAO KWA PAMOJA WALIMVAMIA, KUMJERUHI NA KISHA KUMPORA PIKIPIKI HIYO. 

AIDHA, KUTOKANA NA TUKIO HILO, MTUHUMIWA MMOJA AITWAYE NASIBU KIBONA [23] MKAZI WA MAJENGO AMEKAMATWA BAADA YA WENZAKE HAO WATATU KUKIMBIA NA PIKIPIKI HIYO. JUHUDI ZA KUWATAFUTA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA KITUO CHA AFYA TUNDUMA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUJITAFUTIA KIPATO KWA NJIA HALALI NA KUACHANA NA TAMAA YAN MALI KWA NJIA ZISIZO HALALI.

KATIKA TUKIO LA PILI:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA WA NCHINI UGANDA WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. GODFREY KIIZA [38] AKIWA NA PASIPOTI NAMBA B. 1236110 NA 2. DICKSON LUKYUMUZI [27] AKIWA NA PASIPOTI NAMBA B 12134391 WOTE WAKAZI WA JIJINI KAMPALA WAKIWA NA SILAHA/BASTOLA AINA YA NORINCO YENYE NAMBARI 01596413236 NA RISASI 14.

WATUHUMIWA KWA PAMOJA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 22.11.2015 MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI HUKO ENEO LA UKAGUZI MPAKANI KASUMULU, KATA YA NJISI, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. 

AIDHA, WATUHUMIWA HAO BAADA YA KUPEKULIWA WALIKUTWA NA FUNGUO MMOJA WA PINGU, FUNGUO MBALIMBALI ZA MAGARI NA MILANGO. WATUHUMIWA WALIPEKULIWA WAKATI WANAVUKA NCHINI KUELEKEA NCHINI MALAWI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad