JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


RAIS KIKWETE AMTEUA PROFESA MBETTE KUWA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA KAMPUNI YA SIMU TANZANIA

Share This
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAWASILIANO SAYANSI NA TEKNOLOJIA 
TAARIFA KWA UMMA 
UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA KAMPUNI YA SIMU TANZANIA 
        Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Prof. Tolly Salvatory Augustin Mbwette  kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kipindi cha miaka miaka mitatu kuanzia tarehe 12 Oktoba 2015. 

Uteuzi huo ni kwa mujibu wa kifungu Na. 9 (4) (a) cha Sheria Na. 20 ya Mwaka 1993 iliyoanzisha Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Prof. Tolly Salvatory Augustin Mbwette amekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia tarehe 13 Aprili 2005 hadi tarehe 13 Aprili 2015. Pia amekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa taaluma ni Mhandisi ujenzi aliyobobea kwenye maeneo ya Mazingiria, TEHAMA, Utawala na Menejimenti kwa zaidi ya miaka 25 na amesoma Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam, Tanzania; IHE Delft, Netherland; na Chuo Kikuu cha London, Uingereza kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza, Uzamili na Uzamivu. Pia ameshirikiana na Vyuo Vikuu mbali mbali duniani kutoka Bara la Ulaya, Amerika, Asia na Afrika katika maeneo ya uhandisi, utafiti, TEHAMA, uandishi wa vitabu na majarida mbali mbali.
Imetolewa na:

KATIBU MKUU

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad