JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MRADI WA VETA, VSO NA LNG TANZANIA WASHINDA TUZO YA BRITISH GAS

Share This
Tuzo iliyotolewa kwa Mradi wa EEVT baada ya kupata ushindi katika eneo la Mazingira na Huduma kwa Jamii.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa BG Bw. Helge Lund akizungumza na washiriki wa hafla hiyo ya kutunuku tuzo kwa washindi iliyofanyika Kensington Palace nchini Uingereza hivi karibuni.
 Mkurugenzi wa VETA kanda ya Kusini Mashariki Joseph Kibehele (watatu kutoka kushoto) akiwa ameshikilia tuzo hiyo katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa BG Bw. Helge Lund (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Meneja uwekezaji kwa jamii wa LNG Tanzania Bi. Kate Sullam, Mwakilishi kutoka LNG Tanzania Bi. Patricia Muhondo, Meneja Mradi wa Hali Bora ya Maisha (Livelihood) wa VSO Bi. Rose Tesha na mmoja wa majaji wa shindano hilo.
 Washiriki kutoka nchi mbalimbali walioshiriki katika hafla hiyo katika picha ya pamoja wakati wa chakula cha jioni.



MRADI wa Kuongeza Sifa za Kuajirika kupitia Mafunzo ya Ufundi Stadi (EEVT) unaoendeshwa kwa ushirikiano kati ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), shirika la VSO na Kampuni ya Gas LNG nchini Tanzania umepata ushindi kwa mwaka 2015 katika eneo la Mazingira na Huduma kwa Jamii.

EEVT ilitangazwa mshindi miongoni mwa kundi la washiriki wanne bora walioingia fainali kwenye eneo la Mazingira na Huduma kwa Jamii wakati wa halfa ya kutunuku tuzo iliyofanyika Kensington Palace nchini Uingereza tarehe 12 Novemba, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Afisa Mtendaji Mkuu wa BG Bw. Helge Lund.

Tuzo za BG hutolewa kila mwaka kwa kubaini, kushirikishana na kusherehekea mwenendo ulio bora miongoni mwa washirika wa BG.

Mchakato wa Tuzo za mwaka 2015 ulihusisha washiriki 147 kutoka nchi mbalimbali na wakiwa katika makundi matano ya Ushirikiano katika Kazi; Mazingira na Huduma kwa Jamii; Uthabiti na Ubora katika Utendaji Kazi; Utendaji kazi kwa Usalama na Uadilifu katika matumizi ya Rasilimali; na Ugunduzi. Washiriki wanne bora kutoka kila kundi walichaguliwa kuingia katika kinyang’anyiro cha mwisho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad