JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MASHABIKI WA WASANII WAMETAKIWA KUONDOA ITIKADI ZA VYAMA ZILIZOTOKANA NA KAMPENI

Share This
 Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SHIRIKISHO la Wasanii nchini  wamewataka mashabiki wao kuondoa tofauti  za kiitikadi ambazo zilijitokeza  katika kampeni waendelee kuwaunga mkono.

Akizungumza na waandishi wa habari,mmoja wa msanii, Stara Thomas amesema kila watu walikuwa na itikadi katika kampeni hivyo ni wakati mwafaka wa kufanya kazi.

Stara amesema wameshiriki katika kampeni zimeisha sasa ni wakati kushiriki katika majukumu kama wasanii.

Hata hivyo amesema wanapongeza Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa na watanzania  katika kuongoza.

Nae Msanii Mkongwe, John Kitime amemtaka Rais kuwekea umuhimu wa idara ya utamaduni  kuweza kufanya wizara kutokana na kuwepo kwa changamoto nyingi kwa wasanii.

Kitime amesema idara hiyo kuhama hama kumewafanya wasanii kuwa nyuma na kufanya nchi kushindwa kupata mapato licha ya wasanii kuwa wengi.

Kwa upande Mkurugenzi wa Bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka ameshauri Rais mpya katika uteuzi wa bodi wasanii wateuliwe kutokana na uwezo wao katika kazi hiyo.

Asha amesema kuteuliwa kwa wasanii katika bodi zenye sanaa nchini zitaleta chachu na wasanii watatambuliwa na jamii kwa mchango wao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad