JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


KUMBUKUMBU

Share This
SIMON S. KAHEMELE
26th Julai 1965 – 14th Novemba 2014
Ni mwaka mmoja sasa tangu ulipotuacha ghafla katika ajali ya gari. 

Tukiwa tungali na majonzi ya kuondokewa nawe katika ulimwengu huu, mambo mema uliyotufanyia ulipokuwa hai bado yanaendelea kugusa maisha yetu. 

Tunakukumbuka sana kila iitwapo leo na nyakati tulizoshirikiana hazijafutika katika mioyo yetu. Mke wako, familia yako na marafiki zako wanakupenda sana na kusikia upweke kwa kuondokewa nawe. 
Leo tumekusanyika Manda mahali ulipolala, ili kumshukuru na kumtukuza Mungu kwa kutupa zawadi ya maisha yako hapa duniani na kwa kufungua rasmi kanisa (Simon’s Memorial Chapel), hii ikiwa ni ukamilisho wa ndoto uliyokuwa nayo.  
Shukrani za pekee ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wote walioshirikiana nasi katika kufanikisha ndoto hiyo. Mungu awazidishie pale palipopungua.
 Daima Tunakukumbuka, Pumzika kwa Amani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad