JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


ACT WAZALENDO WAMWOMBA RAIS MAGUFULI KUAMURU ZEC KUTANGAZA MATOKEO ZANZIBAR

Share This
CHAMA Chama cha ACT Wazalendo kimemwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John  Magufuli  ahakikishe Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) itangaze matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu ili walioshinda watangazwe na waapishwe kwaajili ya kuanza kazi katika serikali ya Zanzibar ikiwa mpaka sasa  Zanzibar haina Serikali.

Zitto amesema kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) hakuwa na mamlaka yoyote ile katika tume hiyo ya kukufuta  matokeo ya uchaguzi Zanzibar  kwani tume inawajumbe wake yeye peke yake hana mamlaka hayo.

Pia zitto amesema kuwa chama chake kitafanya kazi kwaajili ya masrahi ya wananchi  ya sasa na yabaadae, pia amesema kuwa chama chake hakitashiriki katika kugombea nafasi ya spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.














Aliyekuwa mgombea wa Urais, Anna Mgwira   akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mwenendo wa siasa ulivyofanyika hapa nchini pamoja na kuwashukuru baadhi ya waandishi wa habari kwa kuripoti habari waliojitokeza katika kampeni bila kujari itikadi zao katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwao jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini  kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kushinda kwa chama chake katika jimbo la Kigoma Mjini pamoja na Kuongoza kupata madiwani katika kata 50 hapa nchini na katika  Manispaa ya Kigoma Ujiji kufanikiwa kuunda baraza la madiwani  ikiwa  Manispaa hiyo ina kata 18  chama cha ACT-Wazalendo  kushinda na kupata madiwani 12 na CCM ikipata kata 5 na  Chadema kata 1 ikiwa kata moja haikufanya uchaguzi na itafanya Jumapili Ijayo.
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha ACT -Wazalendo, Samson Mwigamba katikati ni aliyekuwa mgombea wa Urais wa chama cha ACT-Wazalendo,Anna Mgwira na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini  kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano na viongozi wa chama cha ACT-Wazalendo jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad