JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WATAKIWA KUCHANGIA UJENZI WODI YA AKINAMAMA

Share This
Mgombea Ubunge kushoto Ridhiwani Kikwete akimkabidhi ilani ya uchaguzi ya CCM mgombea udiwani wa kata ya Kimange wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani kwenye kata hiyo katika Kijiji cha Pongwekiona 

Na John Gagarini, Chalinze
WAKAZI wa Kijiji cha Pongwe Kiona Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo wametakiwa kushirikiana na serikali ili kukamilisha ujenzi wa wodi ya akinamama.

Hayo yalisemwa na mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete kwenye Kijiji hicho wakati wa uzinduzi wa kampeni za Udiwani kwenye kata ya Kimange na kusema kuwa kwa sasa hakuna wodi ya akinamama.

Ridhiwani alisema kuwa moja ya vitu ambavyo amevipa kipaumbele ni upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na huduma ya afya ya uzazi ya mama na mtoto ili waweze kuhudumiwa kwa uhakika.

“Nawaombeni wananchi tuungane na serikali kwa kuchangia nguvu zetu kuhakikisha wodi ya akinamama inakamilika kwani kwa sasa hakuna hata chumba cha kujifungulia ambapo wanapojifungua wanachanganyika na wanaume jambo ambalo linasababisha kutokuwa na utu wa mwanamke,” alisema Ridhiwani.

Alisema kuwa heshima ya mwanamke inapotea kutokana na kutokuwa na wodi hiyo ambayo ingewafanya akimama kuweza kujifungulia sehemu ambayo ina wastiri tofauti na ilivyo sasa hakuna stara kwa wanawake.

“Nawaomba mnichague ili niweze kuwa Mbunge wenu niweze kuhamasisha ujenzi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo name nitahakikisha ujenzi huu unakamilika kwa wakati ili kuondoa adha wanayopata akinamama wakati wa kujifungua,” alisema Ridhiwani.

Kwa upande wake Mgombe Udiwani Hussein Hadingoka alisema kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha anahamasisha wadau mbalimbali kuweza kuchangia ujenzi huo ambao tayari umeashaanza na uko kwenye hatua ya msingi.

Hadingoka alisema kuwa mbali ya ujenzi huo pia atahakikisha ujenzi wa zahanati za Vijiji kwenye kata hiyo unafanyika kwani baadhi ya vijiji havina zahanati hali ambayo inasababisha changamoto ya wananchi kwenda mbali kupata huduma za kiafya huku ilani ya chama ikisema kuwa kila kijiji kitakuwa na zahanati na kata kuwa na kituo cha afya.

Naye mkazi wa Kijiji hicho Asha Bakari alisema kuwa wodi hiyo ikikamilika itakuwa imewaondolea adha ya kujifungua huku wanaume nao wakiwa kwenye chumba kimoja ambapo hadhi ya mwanamke inapotea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad