JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WAANDISHI WAMETAKIWA KUTAJA MAJINA SAHIHI YA WATU WENYE ULEMAVU KUEPUKA UNYANYAPA

Share This
 Mwezeseshaji wa mafunzo ya waandishi wa habari katika uchaguzi jumuishi,kwa watu wenye ulemavu,Blandina Sembu akizungumza na waandishi wa (habari hawapo pichani) juu ya waandishi kuhamasisha watu wenye ulemavu kupiga kura katika mazingira rafiki katika semina iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya waandishi wakifatilia maada katika semina iliyoandaliwa  na SHIVYAWATA BA panoja na Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam(DCPC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
WAANDISHI wa habari wametakiwa kuandika habari kwa usahihi wakiwataja watu wenye ulemavu kwa kutumia majina sahihi kuepuka unyanyapa dhdi yao .

Rai hiyo ilitolewa juzi jijini Dar es Salaam na Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Lucas Kija, wakati wa mafunzo ya siku mbili ya waandishi wa habari juu ya uandishi wa habari za uchaguzi kwa watu wenye ulemavu.

Mafunzo hayo ambayo yaliwashirikisha waandishi wa habari kutoka Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Kilimanjaro na Tanga  yaliandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari wa Jiji la Dar es Salaam (DCPC),  kupitia Mradi wa Uchaguzi Jumuishi.
"Kuna majina sahihi na yasiyo sahihi kwa watu wenye ulemavu, hivyo waandishi wa habari lazima mtaje mhusika kwa kutumia jina sahihi," alisema Kija alipokuwa akitoa mada katika mafunzo hayo.

Kwa mujibu wa mwezeshaji huyo, miongoni mwa majina yasiyo sahihi ni kipofu, wasiosikia, vichaa, chizi, zeruzeru na watu wenye mtindio wa ubongo ambayo hayapaswi kutumiwa.

Mwezeshaji huyo aliyataja baadhi ya majina sahihi yanayopaswa kuwaita watu wenye ulemavu kuwa wasioona, viziwi na walemavu wa akili.

Katika mafunzo hayo, washiriki walipata fursa ya kupata elimu kuhusu vikwazo vikuu vinavyokwamisha ushiriki wa watu wenye ulemavu katika uchaguzi. Elimu hiyo ilitolewa na Wawezeshaji Kija na Blandina Sembu.

Wawezeshaji hao walisema vikwazo hivyo vimegawanyika katika mitazamo ya kijamii, mazingira na kitaasisi.

Amesema kuna  vikwazo vya vimekuwepo katika mchakakato wa uchaguzi kunazia kampeni,usalama kutokana na mazingira ya jamii hiyo,kukosekana kwa takwimu sahihi za watu wenye ulemavu, miundombinu isiyo rafiki na sheria kandamizi mfano gharama za uchaguzi.

Kaimu Mkurugenzi wa SHIVYAWATA, Francis Gugu ambaye pia ni mlemavu wa usikivu hafifu, alisema shirikisho hilo linajumuisha vyama 10 vya watu wenye ulemavu kitaifa na limekuwa likifanya ushawishi na utetezi kwa watu wote.
Akizungumzia mradi huo, Gugu alisema Mei 20, mwaka huu, SHIVYAWATA ilitia saini mradi huo wa mwaka mmoja na Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN-Women) kwa lengo la kuchoche ushiriki wa watu wenye ulemavu katika uchaguzi mkuu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad