JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


UDA yaahidi msaada zaidi kwa jeshi la Polisi

Share This
 Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA), Bw. Tumaini Magila (kushoto) akimkabidhi gari namba PT 0828 Toyota Land Cruiser, ASP Charles Hamza (katikati) aliyepokea gari hilo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Pwani, ACP Japhari Mohamed baada ya kazi ya ukarabati wa gari hilo kukamilika.  Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.  Kulia ni dreva, G. 6633 PC Pendael.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) imesema itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kusaidia shughuli za kijamii na taasisi mbalimbali likiwemo Jeshi la Polisi ili kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kujenga taifa bora.

Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa kampuni hiyo, Bw. Tumaini Magila amesema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wakikabidhi gari la Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani ambalo lilifanyiwa matengenezo kwa msaada wa kampuni yao baada ya gari hilo kuwa bovu kwa muda mrefu.

“Tumekuwa tukishiriki kusaidia masuala ya kijamii yakiwemo ya watoto yatima, na taasisi mbalimbali hapa nchini,” alisema wakati wa makabidhiano ya gari hilo lenye namba PT. 0828 aina ya Toyota Land cruiser.

Naye ASP Charles Hamza akipokea gari hilo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ACP Japhari Mohamed aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo.

“Baada ya matengenezo haya, doria zetu zitaimarika,” alisema.

Alitoa wito kwa jamii na kampuni mbalimbali kuiga mfano wa kampuni hiyo katika kusaidia jeshi la polisi katika changamoto zake mbalimbali ili liweze kuendelea na majukumu yake vizuri.

Alisema ulinzi wa watu na mali zao ni jambo la msingi ambapo kila mmoja anatakiwa kuunga mkono juhudi hizo ili kutoa fursa kwa jamii, taasisi na kampuni mbalimbali kufanya shughuli za uzalishaji kwa usalama.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad