Na Mwandishi
Maalum, New York
TANZANIA imetoa wito Kwa Jumuiya ya Kimataifa wa kuhakikisha inashirikiana kuhakikisha kwamba silaha za maangamizi zikiwamo za nyukilia haziiangukii mikono ya
makundi ya kihalifu.
Wito huo umetelewa mwishoni mwa wiki na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi,wakati wa Mkutano kuhusu
masuala ya uponyaji wa silaha na usalama wa kimataifa.
Katika mkutakno
huo wazungumzaji wengi walieleza
wasiwasi wa kuwapo kwa ushirikiano wa karibu kati ya nchi ambazo
zina silaha za nyukilia na zile ambazo
hazina, lakini huku zile ambazo zinamiliki silaha hizo zikiendelea kuziboresha
na kujilimbikizia.
“Ni jambo la kusikitisha, badala ya kuzipungua silaha hizi na hatimaye
kuzitokomeza kabisa, nchi zinazolimiki
silaha za nyukilia zinaendelea na kasi ya kuziboresha , kuzifufua na kujilimbikiza”. Akasema Balozi Manongi.
Akabainisha kuwa mbaya Zaidi hata zile nchi ambazo hazina silaha hizo nazo sasa
zinatafuta kila maarifa ya kuwa nazo. Jambao
ambalo amesema ni tishio kwa usalama wa mwanadamu.
Amesisitiza kuwa ingawa ni miongo saba imekwisha kupita lakini madhara
ya matukio ya Hiroshima na Nagasaki
bado yanaendelea na yapo hai
miongoni mwetu.
Balozi Manongi akaongeza kuwa ni muhimu basi
utokomezaji wa silaha za nyukilia na teknolojia inayoambatana nazo
likaendelea kupewa kipaumbele pamoja na
kuwa na mikataba ya kisheria itakayosimamia
jambo hilo.
Akasema kutoka na
ongezeko la ulimbikizaji wa
silaha za nyukilia, Jumuia ya kimataifa
inawajibu wa kushirikiana kuhakikisha kwamba silaha hizo na nyingine za
maangamizi haziangukii mikononi mwa
makundi ya kigaidi na kihalifu.
Pamoja na ukweli kwamba silaha za
nyukili na zingine za maangamizi bado ni
tishio kubwa kwa uhai wa mwanadamu. Balozi Manongi akasema kwa nchi
zinazoendelea tatizo la usaambaji na
matumizi holela ya silaha ndogo na nyepesi
zinaendelea kuwa janga kubwa kwa ustawi na maendeleo ya bara hili na
kwingineko.
Akimnukuu Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa
Mataifa Kofi Annan kwamba madhara yatokanayo na matumizi
holela ya silaha ndogo na nyepesi
yameendelea kuwa makubwa sana na
madhara yake ni makubwa pengine
kuzidi mabomu ya atomic
yaliyoiangamizia Hiroshima na Nagasaki.
Akizungumzia zidi kuhusu matumizi
holela ya silaha ndogo na nyepesi,
Mwakilishi huyo wa Tanzania
anasema mirindimo ya risasi na hata matumizi ya silaha kali zikiwamo za
maangamizi, haiwezi au haitamhakikishia mwananchi maisha yenye hadhi, utu, ustawi na
maendeleo.
Akasema kuna uhusiano mkubwa baina ya Amani, usalama na utekelezaji wa Malengo ya
maendeleo endelevu y (Agenda 2030) malengo yanayojikita katika kumaliza umaskini pasipo kumwacha yoyote nyuma pamoja
na kuilinda sayari dunia.
Akasema itakuwa
vigumu kuyatekeleza malengo mapya
ya maendeleo kama kiwango cha gharama
za kujilimbikiza silaha kitaendelea ambapo inakadiriwa kuwa mataifa hasa yale makubwa yanatumia Zaidi ya dola za kimarekani trillion 1.7 kwa mwaka kwa matumizi ya silaha.
Akasema matumizi ya kiasi hicho cha fedha
kujilimbikizia silaha katika maghara mbalimbali duniani huku mamilioni ya watu wakiendelea kuishi
katika umaskini uliopindukia, na maelfu
ya watoto wakiathirika kwa utapia mlo na wengine wakipoteza maisha kwa
kukosa chakula na huduma nyingine za
msingi ni jambo lisilo kubalika.


No comments:
Post a Comment