JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


SHINDANO LA SERENGETI MASTA LAHITIMISHWA JIJI LA MBEYA NA ARUSHA

Share This
Mshiriki wa shindano la kumsaka Serengeti Masta wa jumla kwa jiji la Mbeya Ibrahimu Allam aliyetokea baa ya Liz Pub iliyopo Mafiat jijini Mbeya akinywa bia ya Serengeti Premium Lager kabla ya kuingia kwenye mchuano wa kumpata mshindi wa jumla wa kampeni ya Serengeti Masta kwa jiji la Mbeya uliofanyika kwenye baa maarufu ya Mbeya Pazuri iliyopo Sae jijini humo mwishoni mwa wiki. Kampeni hiyo imefikia tamati jijini Mbeya baada ya kudumu kwa takribani miezi miwili ikizunguka baa kwa baa kusaka washindi mbalimbali wanaotambua ladha halisi ya bia hiyo lakini pia imetoa elimu kwa wateja wake kuhusiana na chapa hiyo namba moja kutoka SBL.


Mshindi wa jumla wa shindano Serengeti Masta kwa jiji la Mbeya Faraji Mbwambo kutoka baa ya Gambino jijini Mbeya akionesha kitita cha fedha sh. 100,000 alizotunukiwa baada kuibuka mshindi wa jumla wa kuitambua ladha ya bia ya Serengeti Premium Lager kati ya vinywaji vitano vinavyozalishwa na kampuni ya SBL. Kampeni hiyo ya Serengeti Masta imewakutanisha wateja na mameneja wa bia hiyo katika kujifunza kwa undani kuhusiana na bia hiyo ambapo mameneja hao walitoa zawadi mbalimbali kwa washindi walioweza kuitambua ladha halisi ya bia hiyo katika kipindi cha kampeni.
Mshiriki wa shindano la Serengeti Masta na mkazi wa Arusha Sebastian Michael akionja ladha tofauti za bia zilizo mbele ya meza yake ili kuitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti Premium Lager katika shindano la kumpata Serengeti Masta wa mkoa wa Arusha ambalo lilifanyika katika Baa ya Bondeni, Kijenge juu jijini Arusha mwishoni mwa wiki hii. Shindano hilo linalodhaminiwa na bia ya Serengeti Premium Lager limewakutanisha wapenzi mbalimbali wa bia hiyo huku likitoa elimu juu ya bia yake na zawadi mbalimbali kama fedha fulana na bia za bure katika kipindi chote cha miezi miwili jijini humo.
Mshindi wa jumla wa shindano la Serengeti Masta kwa wakazi wa Arusha Laota Elias akionyesha fedha taslim Tsh. 100,000/= alizopokea wakati wa shindano la mwisho la kumtafuta “Serengeti Masta” wa jumla wa mkoa huo lililofanyika katika baa ya Bondeni iliyopo Kijenge juu jijini Arusha. Ushindi wa jumla wa Bw. Elias umekuja baada ya kuwabwaga washiriki wenzake watatu katika mtanange wa mwisho wa kuitambua ladha halisi ya bia hiyo na kuibuka “Serengeti Masta” wa mkoa wa Arusha. Shindano hilo la “Serengeti Masta” limezunguka katika baa mbalimbali za jiji la Arusha likiwaburudisha wateja wa bia hiyo na kuwafundisha wahudumu wa baa mbalimbali juu ya utoaji huduma kwa wateja.


Mmoja wa washiriki wa shindano la kumtafuta Serengeti Masta wa jiji la Mbeya akitokea Power bar ya Mbalizi Maxmilian Majaliwa Kamanga akijaribu ladha tofauti za vinywaji vya kampuni ya SBL katika baa ya Mbeya Pazuri ambapo shindano la mwisho la kumtafuta mshindi wa jumla kwa mkoa huo lilifanyika mwishoni mwa wiki. Shindano hilo limezunguka katika baa mbalimbali jijini humo ambapo kwa ujumla shindano hilo limewafikia wahudumu zaidi ya 4000 Tanzania nzima katika kipindi cha miezi miwili ya kampeni na kuwafunza juu ya utoaji huduma kwa wateja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad