JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


PAPA WEMBA KUTUMBUIZA TAMASHA LA KARIBU MUSIC FESTIVAL NOVEMBA 6-8 MWAKA HUU

Share This
 Ofisa Mauzo wa Karibu Cultural Promotions Organization (KCPO), Ernest Biseko katikati  ambao ni waratibu wa Tamasha la Karibu Music Festival akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. kushoto ni  ni msanii, Jhikolabwino Manyika - Jhikoman na Meneja Uvumbuzi wa kinywaji cha Jebel cha Kampuni ya SBL, Attu Mynah
 Msanii Jhikolabwino Manyika - Jhikoman   wasanii wa Tamasha la Karibu Music Festival walivyojiandaa na  akionesha umahiri wake wa kupiga gitaa mbele ya waandishi wa habari  leo jijini dar es saalam
 Baadhi ya waandishi wa  habari
Jhikolabwino Manyika - Jhikoman (kulia) akionesha ufundi wake wa kuimba na gitaa kwa wanahabari leo baada ya mkutano.
Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

MWANAMUZIKI nguli wa dansi kutoka nchini Congo DR, Papa Wemba ni miongoni mwa wasanii wanaotarajia kutumbuiza katika tamasha kubwa la Kimataifa la Muziki la 'Karibu Music Festival' linaloratibiwa na Karibu Cultural Promotions Organization (KCPO) na Legendary Music Entertainment and Promotions Co. Ltd. 

 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Ofisa Mauzo wa KCPO, Ernest Biseko alisema wanamuziki wengine na bendi zinazotarajia kutumbuiza katika tamasha hilo ni pamoja na Sarabi Band, H-Art The Band, Yuzzo & Frontline Band. 

Alisema wasanii kutoka Tanzania watakaotumbuiza ni pamoja na Jhiko Manyika (Jhikoman) na band yake ya Afrikabisa, Tomgwa Ensembe, Misoji Nkwambi mshindi wa BSS 2008, Ze Spirit. 

Isha Mashauzi, Damian Soul na babd yake, Juma Nature, Msafiri Zawose na band yake. Akifafanua zaidi Biseko alisema tamasha hilo la mwaka huu lenye kauli mbiu ‘Fahari ya Tanzania’ litafanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia Novemba 6 hadi 8 mwaka huu katika viwanja vya Mwanakalenge karibu na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA). ".

Tamasha hili linalenga kukuza muziki wa Kiafrika na kuonesha tamaduni za Kiafrika kwa dunia nzima kupitia jukwaa la muziki litakalokutanisha wanamuziki kutoka sehemu mbalimbali duniani," alisema Biseko.

 Aidha alibainisha kuwa tamasha hilo ni sehemu ya kukutanisha wadau wote wa muziki kutoka dunia nzima, kubadilishana uzoefu wa kikazi na kufungua milango kwa wasanii kukuza mtandao wa marafiki na kujifunza vitu vipya toka wasanii wa je ya Nchi. Aliongeza kuwa wanamuziki wote watakaopanda jukwaani siku zote tatu za tamasha watatumbuzia na vyombo vyao 'live' na hakutakua na kutumia CD (playback). 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad