Wachezaji wa timu ya EFM na timu ya Magogoni Veteran katika uwanja wa shule ya msingi Ufukoni.
Wakazi wa kigamboni wakishuhudia mechi kati ya EFM na Magogoni Veteran kigamboni.
Mamia ya watu waliojitokeza kushabikia kabumbu kati ya 93.7 EFM na Magogoni Veteran Kigamboni.
MUZIKI mnene Bar kwa Bar wiki iliyopita ulivuka kivuko na kuhamia Kigamboni,wakazi wa eneo hilo ambao ni wasikilizaji wa 93.7 EFM walipata burudani ya aina yake kutoka kwa timu nzima ya EFM redio.
Burudani ilianza na kabumbu katika uwanja wa shule ya msingi Ufukoni kati ya EFM na magogoni veteran,Timu ya magogoni veterani ilitetea ushindi nyumbani kwa kuifunga EFM magoli manne huku EFM ikiambulia mawili 2.
Kwa kuwa kigamboni kumezungukwa na fukwe kibao, muziki mnene uliendelea katika fukwe ya Navy beach. Rdj’s walishusha ngoma kali na kuwapagawisha wakazi wa kigamboni kwa burudani ya kihistoria.
Baada ya pwani ni zamu ya Dar-es-salaam hivo wakazi wa jiji hili wajiandae kwa kuwa tutawafikia na kuwapa burudani ya kihistoria alisema Denniss Ssebo mkuu wa idara ya mahusiano EFM.
No comments:
Post a Comment