JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MSANII WA NCHINI KENYA,FRASHA KUTUMBUIZA IJUMAA HII JIJINI DAR

Share This
 Msanii wa mziki wa Hip hop wa nchini Kenya ambaye pia ni Daktari nchini humo, Francis Hamis ( a.k.a Frasha) akizungumza leo katika mkutano uliofanyika katika ukumbi uliopo katika jengo la VIVA Tower na waandishi wa habari kuhusiana na kutumbuiza kesho Ijumaa ambapo baada ya kutumbuiza atatembelea vituo kadhaa vya watoto yatima hapa jijini Dar es Salaam ataanza na kituo cha Trust youth Care pia mesema kuwa kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu 10 kwa kabla ya saa  sita usiku na baada  ya saa sita kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu 15 atatumbuiza katika ukumbi uliopo katika jengo la VIVA TOWER jijini Dar es Salaam. Nyimbo atakazo tumbuiza ni WekaWeka Kutibu pamoja na Dalia.
Kulia ni Meneja mauzo wa kinywaji cha Johnnie worker, Francis Tibaikana akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na vinjwaji vitakavyokuwepo wakati wa msanii Frasha akitumbuiza amesema kuwa chupa moja ya kinjwaji cha Johnnnie Worker itauzwa kwa shilingi laki moja na elfu idhirini badala ya shilingi  laki moja na elfu hamsini. Pia aliwaalika watanzania kuhudhulia wakati wa msanii huyo akitumbuiza na kujipatia ofa za pumbuzo la bei la kinywaji cha Johnnie Worker ikiwa msanii huyo atatumbuiza katika ukumbi uliopo katika jengo la VIVA TOWER jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad