JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


MGODI WA DHAHABU WA GEITA (GGM), UMEZALISHA AJIRA ZAIDI YA 200

Share This
 Mwandishi Wetu, Geita
MGODI wa dhahabu wa geita (GGM), umezalisha ajira zaidi ya 200 kwa jamii baada kuwekeza zaidi ya Sh1.7 Bilioni kupitia programu ya Uchumi na Maendeleo (GEDP) ambayo imelenga kusaidia wakulima na wajasiriamali wadogo na wa kati, wanaoishi jirani na mgodi.

Akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Geita, Fatma Mwassa alipotembelea mgodini hapo juzi, Makamu wa Rais wa Anglo Gold Ashanti/GGM, Simon Shayo alisema mpango umelenga kubadili hali za maisha ya wakazi kuwa tofauti na ilivyokuwa kabla mgodi haujaanza kufanyakazi.

Alisema mradi umewasaidia wakazi hao na familia zao kuwa na fani ambazo wanazitumia kwa uzalishaji na mbinu za kujipatia masoko katika mji wa Geita na maeneo mengine nje ya mgodi huo.

"Hiyo inatokana na ubora wa mafunzo ambayo tunawapa sanjari na mbinu za biashara" alisema meneja huyo na kuongeza kuwa zaidi ya ekari 800 zimetengwa kwa ajili ya kilimo cha Alizeti, Mpunga na mazao mengine na utafiti wa udongo umekamilika.

Pia utengenezaji wa miundombinu kwa ajili ya umwagiliaji unafanyika na upande mwingine, ununuzi wa mashine za umwagiliaji, uchomeaji, mashine za kuzalisha umeme, vyerehani na mashine za kudarizi kwa ajili ya wananchi hao wa Geita vinafanyika.

Meneja huyo alibainisha kuwa lengo ni kuhakikisha kunakuwa na mnyororo endelevu wa thamani ya mazao ya kilimo kwa kuongeza viwango vyao vya ufahamu katika mfumo wa masoko na kuongeza ubora wa mazao na wigo wa biashara kwa wajasiriamali hao wadogo na kati.

"Tunatumia programu hiyo kwa ajili ya kuwawezesha wakazi iuchumi na pia kupunguza kiwango cha umaskini" anasema na kuongeza kuwa mpango huo utapunguza idadi ya vijana wasio na ajira Geita na wengine ambao wamekuwa wakijitumbukiza katka uhalifu mgodini.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Fatma Mwassa alisema kuna matumaini makubwa kuwa jitihada hizo za GGM zitazidi kukua na kubadili maisha ya walio wengi kwa kuwawezesha kiuchumi wananchi wa Geita.

"Naamini sasa watauza mazao na bidhaa zilizokamilika na sio ghafi kama awali na sio kwa Geita pekee bali pia nchi jirani" alisema Mwassa. Kulingana na takwimu za hivi karibuni, kilimo kimetoa ajira kwa asilimia 88 ya watanzania nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad