JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


KUDUMISHA AMANI WAKATI WA UCHAGUZI

Share This
WATANZANIA wametakiwa  kuendelea kudumisha amani hasa kipindi  cha uchaguzi kwani bado nchi yetu inasifika kwa amani dunia kote
kauli hiyo imetolewa na  mwanaharakati wa amani Mhonda Joseph wakati akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam.

Mhonda amesema wananchi wahakikishe  amani inakuwepo  na hata  wageni wanaoishi hapa  kutokana na historia ya miaka ya nyuma  ya hapa nchini kuwa ya amani.

Aidha  amewataka watanzania wasikubali  baadhi ya watu  wachache kuja kuchochea utovu wa amani na wakumbuke amani ikipotea ni vigumu kuirudisha pindi itakapotoweka.

lakini pia Mhonda ameeleza kuwa  hatua tuliyofikia ya kuwa na vyama vingi  ni moja ya maendeleo  ni mhimu kuhakikisha  tunachagua kiongozi bora  atakao watumikia watanzania wote kutokana na hali ya ugumu wa maisha kwa  sasa.



hata hivyo amewataka mawakala kuhakikisha wanafanya kazi zao bila kukubali kufanya vurugu pindi wanaposimamia wakati wa kuhesabu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad