JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


KITABU KILICHOTUNGWA NA MTOTO WA KITANZANIA CHANG"ARA KIMATAIFA

Share This
MTOTO wa Kitanzania mwenye miaka 14 ametunga kitabu ambacho kimetambulika kimataifa. Kitabu hicho ni cha hadithi kinachoitwa ''LUCIANA AND THE SEVEN MAGICAL RINGS'' ambacho kimepigwa chapa na kampuni ya Kimarekani inayoitwa KIDPUB PRESS ya mjini Boston. Kinasambazwa pia na kampuni za Marekani za Amazon na Bookstore.

Mtunzi wa kitabu hiki ni Redempta Rugeiyamu ambaye kwa sasa anaishi nchini Afrika Kusini ambaye alizaliwa nchini Botswana walikokuwa wakiishi wazazi wake akiwa na ugonjwa unaoitwa Cerebral Palsy. 

Amekuwa akiishi na ugonjwa huo tangu alipozaliwa miaka 14 iliyopita. Japokuwa ugonjwa huo umeathiri viungo vyake na kumpa taabu ya kutembea na kuongea lakini haukumzuia ndoto yake ya kuandika vitabu, kuimba na kucheza muziki.

Kitabu hicho kilizinduliwa mjini Gaborone na Mwenyekiti wa Chama Cha Watanzania waishio Botswana, Bw. Nieman Kissasi, siku ya jumamosi usiku. Mgeni rasmi kwenye shuhuli hiyo alikuwa ni Balozi wa Tanzania nchini Arika Kusini ambaye aliwakilishwa na Afisa wa Ubalozi, Bw. Elibahati Lowassa.
 Mwenyekiti wa Watanzania Waishio Botswana, Bwana Nieman Kissasi, akizindua rasmi kitabu hicho mjini Gaborone siku ya jumamosi usiku kwenye mkutano mkuu wa Chama hicho. Wengine pichani ni wazazi wa Redempta, Bw. Theo Rugeiyamu na Celina Rugeiyamu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad