JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


BARAZA LA VYAMA VYA SIASA NCHINI WAJADILI MWENENDO WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU

Share This
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Peter Kuga Mziray akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na kutafakari  mwenendo  wa Kampeni unavyoendelea na Changamoto na Utatuzi wake katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Zanzibar,kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Fedha ya Baraza la vyama vya Siasa Constantine Akitanda na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Siasa ya Baraa la vyama vya Siasa Lifa Chopaka.
-Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Peter Kuga Mziray kuhusiana na masuala mbalimbali ya uchaguzi katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Zanzibar.Picha na Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Baraza la Vyama vya Siasa nchini limevishauri vyama vya siasa kuzungumza na kuwasihi wafuasi wao kutii sheria bila shuruti ili kuendeleza amani iliyopo nchini.

Aidha Baraza hilo limeviomba Vyama kuwaeleza wafuasi na wapenzi wao kurudi majumbani na kuendelea na shughuli zao mara baada ya kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu kama ilivyokuwa kwa hatua za uandikishwaji.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Peter Kuga Mziray wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu Kikako maalumu cha Baraza hilo kilichofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.

Kikao hicho kilitafakari mwenendo wa Kampeni za Wagombea katika ngazi mbalimbali na kujadili changamoto mbalimbali na utatuzi wake ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki na kufanyika katika mazingira ya Amani na Utulivu.

Mziray amefahamisha kuwa wamekubaliana katika kikao hicho kuwa Wapiga kura wana haki kama watapenda mara baada ya kura kuhesabiwa na matokeo kubandikwa kwenda Vituoni hapo kwa ajili ya kuangalia Matokeo kwa wakati wanaopenda.

Aidha amesema Vyama pia vimesisitizwa kuweka Mawakala wanaowaamini katika Vituo vya kupigia kura ambao watajumuisha kura za Wagombea katika nafasi za Madiwani, Wabunge na Rais katika maeneo husika.
Mziray ameongeza kuwa Baraza la Vyama vya siasa pia limeshauri Vyama hivyo kuzingatia na kuweka amani ya nchi mbele kwa maslahi ya Taifa.
 “Katiba ya Nchi iko wazi kuwa atakayeshinda kwa kura nyingi ndiye atakayetangazwa na kupewa cheti na Tume ya uchaguzi” alisema Mziray
Ametoa rai kwa Katibu Mkuu kiongozi kuratibu shughuli za kuapishwa Rais ambaye kwa mujibu wa Sheria huapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania mara baada ya kutangazwa ndani ya kipindi kisichozidi siku saba.
Mzirai pia ameelezea kufarijika kwao na Tume ya Uchaguzi kwa kuvihakikishia Vyama vya siasa kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki na kwamba Mgombea atakayeshinda kwa kura nyingi zaidi na halali ndiye atakayetangazwa kuwa Mshindi.

Mzirai amevimetaka Vyama vya siasa kuwaasa Wagombea wao kukubali Matokeo kama yatakavyotangazwa na Tume ya uchaguzi ya kushinda au kushindwa.

 Kwa upande wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mwenyekiti wake Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Mwakilishi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Khamis Khamis wakati wakiwasilisha mada juu ya usimamizi na utekelezaji wa maadili Uchaguzi nchini wamevitaka Vyama vya sias kuendelea kuzingatia maadili ya uchaguzi kwa kuwa shauku ya kila Mtanzania ni kuona uchaguzi unaisha kwa amani.

Kikao hicho maalum cha cha siku mbili cha Baraza la Vyama vya Siasa kilijumuisha Wajumbe kutoka Baraza hilo, Wageni kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC na Jeshi la Polisi na kuandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini.
Baraza la Vyama vya Siasa limeundwa chini ya kifungu 21B cha Sheria ya Vyama vya siasa Namba 5 ya mwaka 1992 kama ilivyorekebishwa na Sheria namba 7 ya mwaka 2009. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad