jlogo

Karibuni Jamvini Wanajamii

topads

Post Top Ad

demo-image

AIRTEL YAZINDUA OFA YA INTANETI BILA KIKOMO

Share This
 Mkuu wa Huduma za Intaneti wa Airtel Tanzania, Gaurav Dhingra
(katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
jana, wakati akizindua ofa kabambe ya “ Yatosha Nyts Intaneti bila
kikomo”, ambayo itamwezesha mteja kuperuzi intaneti bila kikomo wakati
wa usiku kila siku. Kushoto ni Afisa Masoko wa Kitengo cha Intaneti,
Erick Daniel na Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde.
2
 Afisa Masoko wa Airtel Kitengo cha Intaneti, Erick Daniel (kushoto)
akionyesha jinsi ya kutumia huduma ya ofa kabambe ya “ Yatosha Nyts
Intaneti bila kikomo”, ambayo itamwezesha mteja kuperuzi intaneti bila
kikomo wakati wa usiku kila siku, baada ya kuzinduliwa jijini Dar es
Salaam jana. Katikati ni Mkuu wa Huduma za Intaneti wa Airtel
Tanzania, Gaurav Dhingra na Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde.
3
  Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde. (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa
ofa kabambe ya “ Yatosha Nyts Intaneti bila kikomo”, ambayo
itamwezesha mteja kuperuzi intaneti bila kikomo wakati wa usiku kila
siku. Katikati ni Mkuu wa Huduma za Intaneti wa Airtel Tanzania,
Gaurav Dhingra na Afisa Masoko wa Kitengo cha Intaneti, Erick Daniel.


·         Kwa Tsh 600, kuanzia saa 6 usiku hadi 12 asubuhi
Dar es Salaam, Jumatano 7th Oktoba 2015,  Kampuni ya simu za mkononi
ya Airtel leo imetangaza uzinduzi wa ofa kabambe ya “Yatosha Nyts
Intaneti bila kikomo”  kwa wateja wake nchi nzima. Ofa hii ya kipekee
itawawezesha wateja wa Airtel kufurahia kuperusi internet bila kikomo
wakati wa usiku kila siku.

Huduma ya internet imeendelea kuileta dunia karibu, Kupitia huduma za
internet dunia imeletwa karibu na kuwa kijiji kimoja. Takribani
asilimia 42.4 ya watu duniani wanatumia huduma ya intaneti, kati yao
bilioni 2 wanatoka katika nchi zinazoendelea, wakati milion 89
wanatoka katika nchi ambazo hazijaendelea.  Kwa wastani asilimia 34 ya
wakazi katika nchi zinazoendelea wameunganishwa na huduma za intaneti
(kumb. ITU).

Katika shughuli zetu za kila siku ,wakati wa mchana ni vigumu kupata
muda wa kutumia intaneti kwa mambo yetu binafisi, Ofa hii ya yatosha
nights itatupatia fulsa ya kutumia huduma ya inanet na kuunganishwa na
jamii kwa urahisi zaidi  muda jioni.alisema Gaurav Dhingra Mkuu wa
huduma za intaneti. 

 “leo tunawawezesha wateja kufanya shughuli
mbalimbali zikiwemo kuangalia sinema, mpira, kutuma picha na video kwa
marafiki na wapendwa wao, kupata taarifa za habari mbalimbali
zinazotokea duniani na nchni  bila kujali muda na kiasi cha kifurushi
cha data kitakachotumika. Kwa shilingi 600 kuanzia saa 6 usiku mpaka
saa 12 asubuhi tunawawezesha watanzania  nchi nzima kupata intenati
bila kikomo kupitia  Yatosha Nyts”.

Dhingra aliongeza kwa kusema , wateja wanaweza kununua  kifurushi hiki
cha usiku wakati wowote , ili kujiunga mteja anatakiwa kupiga *149*99#
 na kuunganishwa kwenye menu ya Airtel Yatosha , kisha kuchagua 4 ili
kupata Yatosha Nyts and kisha kufata maelekezo.

Airtel Tanzania chini ya huduma ya Yatosha wiki iliyopita ilizindua
ofa ya  Yatosha Nyts inayompatia mteja uhuru wa kuongea na familia,
marafiki, wapendwa na wafanyabishara wenzao bila kikomo kwa shilingi
300. Ofa hii ya intaneti bila kikomo ni mwendelezo wa dhamira ya
Airtel ya kuleta mawasiliano bora na kuwawezesha watanzania nchini



nzima  kutumia huduma za intaneti
Comment Using!!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad