JIACHIE

Karibuni Jamvini Wanajamii

Tangaza Hapa

Post Top Ad


WANAWAKE WAMETAKIWA KUZIMAMA IMARA KATIKA UCHAGUZI

Share This
WANAWAKE wametakiwa kuzimama imara katika uchaguzi ili kuweza kuchukua nafasi za uongozi katika majimbo ,mikoa, wilaya na serikalini ili kufikia malengo .
 
Hayo yameeelezwa na Mwanaharakati wa masuala ya wanawake Zanzibar Siti Abas Ali wakati lipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Kwerekwe Wilaya ya Magharibi.

Amesema  kuwa kuchukua  nafasi za uongozi kwa wanawake kutasaidia kuweza kujikwamua na hali ya kimaisha  pamoja kuzisaidia familia pindi zinapofikwa na matitizona kuweza kuyafanyia ufumbuzi.

Siti aliwataka wanawake wawe makini katika upigaji kura kwa  kuwapigia  wanawake wenzetu na sio kuwazarau kwani kufanya hivyo kutawapa moyo na kuweza kufikia pale walipokusudia.

Aidha  alifahamisha kuwa jamii iachane na  dhana ya kwamba wanawake  hawana uwezo wa kuongea kwani kwa wakati tulionaowanawake wamukuwa  na uwezo mkubwa wa kuongea katika mazingira tofauti.

Nae kwa upande wake Mwanasheria wa ZAFELA Saada Salum Issa ameitaka jamii wazidishe mashirikiano ili kuweza kusonga mbele katika harati za kimaisha . 

Vile vile alisema kuwa kwa kiasi  fulani  wanawake wamepiga hatua kimaendeleo  kielimu, kisiasa, na katika.
Sambamba na hayo amewataka wanawake wasijiweke nyuma na wawe katika harakati za kijishirikisha katika njacha tofauti za kujikwamua na hali ngumu za kimaisha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad