Wananchi mbalimbali wakiwa katika banda la Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), katika maonyesho ya siku ya bahari duniani yanayoadhimishwa kitaifa Mkoani Mtwara Leo, Asubuhi.
Wananchi mbalimbali wakipewa machapishi na mtaalam wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA), wakati walipotembelea banda la Mamlaka hiyo leo asubuhi, wakati wa maadhimisho ya siku ya bahari duniani yanayoadhimishwa kitaifa mkoani Mtwara.
Wananchi mbalimbali wakiwa katika banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kwenye maonyesho ya Siku ya Bahari yanayoadhimishwa kitaifa mkoani Mtwara, kama walivyokutwa leo asubuhi.
Kepteni Emmanuel Marijani kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA), akiwapa wananchi maelezo ya namna boti zinavyotakiwa kujengwa kwa kiwango maalum kimataifa wakati walipotembelea banda la Mamlaka hiyo leo asubuhi katika maadhimisho ya siku ya bahari duniani yanyoadhimishwa kitaifa Mkoani Mtwara.
Mtaalam kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya jamiiMifuko ya Jamii, akiwapa maelezo namna taasisi hiyo inavyofanya kazi katika maonyesho ya Siku ya BAhari Duniani yanayofanyika kitaifa Mkoani Mtwara.
Wananchi wa Mkoani Mtwara, wakimsikiliza Afisa Mteule Daraja la Pili WOII kutoka Kikosi cha Wanamaji, Makao Makuu, Kigamboni, Dar es Salaam, Jackson Kavula, wakati wananchi hao walipotembelea banda la NAVY katika maonyesho ya Siku ya BAhari Duniani, yanayoadhimishwa Kitaifa Mkoani Mtwara.
(Habari Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikali-Uchukuzi)
No comments:
Post a Comment